Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgunda abakishwa timu kubwa Simba kumsaidia Fadlu

Juma Mgunda Sababu.jpeg Juma Mgunda.

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kaimu Kocha Mkuu wa Simba Juma Mgunda amehakikishiwa na mabosi wa timu hiyo ataendelea kubaki katika benchi la ufundi hata ikitokea mabadiliko katika nafasi yake.

Mgunda anawindwa na klabu ya Coastal Union ambayo inamuhitaji kwa ajili ya kujiimarisha kuelekea michuano ya kombe la Shirikisho msimu ujao.

Wakati Simba ikiwa bado haijatangaza hatma ya benchi la ufundi, usajili unaofanyika sasa umetokana na ripoti ya makocha Abdelhak Benchikha na Mgunda ambaye ndiye aliyemaliza msimu akiwa Kocha Mkuu

Litakuwa jambo la kushangaza kama Simba itaachana na Mgunda na kuleta watu wapya katika benchi la ufundi ambao hawafahamu masuala mengi kuhusu klabu.

Na pengine hii ndio sababu uongozi umeona lazima Mgunda abaki hata kama kwa nafasi ya Kocha Msaidizi ikitokea mabadiliko katika nafasi ya kocha mkuu.

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema taarifa kuhusu benchi la ufundi itatolewa wakati wowote kabla ya kikosi kuelekea Misri wiki ijayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live