Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgunda aaminiwe, ana kitu, ataifikisha mbali Simba

Juma Mgunda Sababu.jpeg Mgunda aaminiwe, ana kitu, ataifikisha mbali Simba

Mon, 20 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Kocha Juma Mgunda anapewa timu nilijisemea moyoni kwamba kwa Sasa kuna baadhi ya wachezaji wa Simba wataanza kufanya vizuri. Kwa nini?

Juma Mgunda anaonekana ni Mwalimu anayejua kwamba namna nzuri ya kutengeneza darasa Bora ni kutibu tatizo la saikolojia kwa wanafunzi. Ame'apply hicho kitu kwenye akili za wachezaji wa Simba na matokeo yanaanza kuonekana ingawa bado ni mapema kuona matokeo lakini mwanga upo.

Nahisi jambo kubwa ambalo Mgunda huwa anaongea na Fred ni namna anavotakiwa kujiamini. Tumemuona Fred leo akiwa na shauku kubwa sana ya kupambana tofauti na mechi kadhaa nyuma.

Mabeki wa Dodoma Jiji wamepimwa sana umri, alikua anatoka nyuma akiwania mpira unaodondoka jirani na mabeki wa Dodoma lakini anawapita na kuuwahi mpira ingawa bado Kuna nafasi kadhaa alizipoteza lakini goli lake Moja limeipa ushindi Simba leo.

Huenda kelele za wapenda soka na kuyumba kwa timu ndo kulifanya apotee kwenye jitihada zake lakini Kocha Juma Mgunda nadhani alikua na muarobaini wa saikolojia za wachezaji kwa sasa.

Tofauti iliyopo ni kwamba Benchika ni kocha mwenye profile kubwa Afrika, anahitaji wachezaji wazuri kwenye timu awape maelekezo kitu ambacho kimekosekana Simba kwa takriban misimu mitatu, Juma Mgunda ni kocha ambaye anaweza kuijenga timu kutokana na wachezaji waliopo na akafanya vizuri.

Naamini hilo ndo lililochangia kushusha pressure ndani ya timu na kuamsha ari ya upambanaji.

Ukifuatilia kwa makini hata baadhi ya interview anazofanya Mgunda na vyombo vya habari utagundua ni kocha anayependa kuwapa moyo wachezaji wake kuliko kuwalaumu; jambo hili linafanya morali iamke katika timu.

Huenda Fred huyu huyu anayebezwa na wengi akawa Bora zaidi ya sasa akiongeza kujiamini na kuziba masikio pamoja na kuendelea kuaminiwa.

Kuna wakati wachezaji huwa wanapotezwa na kelele za mashabiki jambo ambalo makocha wengi huwa hawalitilii maanani hadi wachezaji wanapotea na kutemwa, kitu ambacho Mgunda anaonekana kukizingatia.

Nadhani Kocha Juma Mgunda akiaminiwa zaidi au kupewa timu kwa muda mrefu zaidi ataitengeneza timu nzuri sana.

Ikumbukwe Fred Michael huyuhuyu alitoka Green eagles ya Zambia akiwa amecheza mechi 18, magoli 14 na assist 4. Tangu afike Simba January mwaka huu ana magoli 6 ya ligi kuu na hajaanza mechi zote pia ni mechi chache sana alizocheza kwa dakika 90.

Kutokana na mahitaji ya timu yalivyo kwa sasa ni ngumu sana kwake kukubalika kiwepesi lakini kuna taa anaiwasha Fred Michael Koublan.

Wengi sana wanaimarika chini ya Mgunda, Kuna Chasambi, Duchu, Mwenda, Balua na wengine. Hii tu ni ishara kwamba anajua namna ya kuongea nao kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live