Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgunda: Tutafanya maboresho makubwa Simba

Mgunda Simba Gd Mgunda: Tutafanya maboresho makubwa Simba

Thu, 6 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Simba kugotea nafasi ya tatu msimu wa 2023/24 na pointi zake 69 kibindoni benchi la ufundi limebainisha kuwa kuna maboresho makubwa yanakuja hivyo timu mpya inasukwa kwa ajili ya kurejea kwenye ushindani.

Ikumbukwe kwamba ni Juma Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba alibeba mikoba ya Abdelhak Benchikha aliyebwaga manyanga huku mchezo wake wa mwisho kukaa benchi alishuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Yanga 2-1 Simba.

Mgunda amekaa benchi kwenye mechi tisa akiambulia ushindi kwenye mechi 7 na sare mbili zote ilikuwa ugenini, Namungo 2-2 Simba ulikuwa mchezo wa kwanza kuongoza akishuhudia Willy Onana akifunga bao la uongozi na Kagera Sugar 1-1 Simba ilikuwa sare yake ya pili, Uwanja wa Kaitaba.

Funga kazi ilikuwa ni Mei 28 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 2-0 JKT Tanzania huku mwamba Onana akifunga bao la pili kwenye mchezo huo ikiwa ni funga kazi mazima 2023/24.

Mgunda ambaye ndiye bosi wa benchi la ufundi Simba kwa sasa amesema: “Nimeongoza timu kwenye mechi 9 kuna masuala ya kiufundi ambayo yatafanyika hasa maboresho kwa wakati ujao. Tunatambua kwamba ili timu ifanye vizuri lazima kuwe na maboresho hivyo Simba mpya inakuja."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live