Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgunda: Tupo tayari kuifunga Yanga leo

Newslite1666517491860 Mgunda Kocha Mgunda

Sun, 23 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa muda wa Klabu ya Simba SC, Juma Mgunda, amesema kuwa maandalizi ya mchezo wa Derby dhidi ya Yanga SC yamekamilika na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri.

Mgunda amesema utakuwa mchezo mgumu wa ushindani lakini wamejipanga vizuri kuhakikisha wanashinda na kuchukua alama tatu muhimu.

Mgunda ameongeza kuwa katika mchezo huo Simba itaendelea kuwakosa Shomari Kapombe na Jimmyson Mwanuke ambao bado wanaendelea kuuguza majeraha yao.

“Mchezo utakuwa mgumu, lakini sisi tumejiandaa kuhakikisha tunashinda na kupata alama tatu huku tukicheza aina yetu ya mpira tulioizoea. Mechi ya Derby ni ngumu lakini tuko tayari,” amesema Mgunda.

Kwa upande wake Nahodha Msaidizi Mohamed Hussein, amesema kuwa kwa upande wao Wachezaji wapo kwenye hali nzuri na morali ipo juu kuhakikisha wanapata ushindi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live