Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgunda: Simba sio ya kwanza kuboronga, hata Ulaya inatokea

Juma Mgunda   .jpeg Kocha Mgunda

Wed, 29 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kaimu Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Juma Mgunda amewataka mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kukaa pamoja na kutafakari kuhusu hatma ya timu yao na namna ya kuiboresha zaidi kuelekea msimu ujao baada ya kufanya vibaya msimu huu.

Mgunda amesema hayo baada ya kutamatika kwa Ligi Kuu msimu huu na Simba kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo huku ikiangukia kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu ujao badala ya Ligi ya Mabingwa ambayo wamekuwa wakicheza kwa takribani misimu 6.

“Kabla msimu kuanza kila timu inakuwa na malengo yake na klabu ya Simba ilikuwa na malengo yake, lakini hayakufikiwa kwa sababu tumechukua nafasi ya tatu. Ninaamini kuteleza si kuanguka.

“Na kwa matokeo haya, niwaombe mashabiki wa Simba iwe ni wakati wa kutafakari kwa nini tumefika huku, tuliteleza wapi na kwa nini na nini cha kufanya ili msimu ujao tujipange na kurekebisha tulipokosea. Njia yoyote haiwezi kuwa imenyooka. Linapotokea jambo kama hili sio kunyosheana vidole ni kukaa na kutengeneza Simba yetu.

“Kuna vitu ambavyo vimetokea, sisi kama benchi la ufundi, wachezaji, viongozi, mashabiki na wanachama wote kwa umoja wetu tukae chini tuone wapi tumeteleza. Matokeo kama haya si mara ya kwanza kutokea kwetu hata timu kubwa hutokea huko Ulaya,” amesema Mgunda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live