Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgunda: Nitarejesha Simba kwenye makali yake

Mgunda Simba Wd Mgunda: Nitaisaidia Simba

Wed, 8 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

kaimu Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Juma Mgunda amesema kuwa anaamini ataisaidia timu hiyo kurejea katika makali yake ambayo imeyapoteza kwa siku za hivi karibuni baada ya kutetereka na kutopata matokeo chanya.

Mgunda ambaye amechukua mikoba ya Benchikha amesema hayo leo wakati akizungumza kwenye mkutano na wanahabari kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Azam Fc.

"Tunakutana na Azam FC, mchezo utakuwa mgumu sana na tunaweza kusema ni fainali kwa sababu ndio unaotoa taswira ya kushika nafasi ya pili kwa sababu tunahitaji kumaliza kwenye nafasi hiyo.

"Si rahisi, lakini naamini nitaisaidia Simba SC irudi kwenye ushindani, nina imani wachezaji watairudisha timu sehemu nzuri. Vijana waliopo wote wamepevuka na wanaelewa namna ya kufanya ili kuiweka timu katika ushindani, hivyo cha muhimu ni kuwajenga kisaikolojia na kuwarudisha kwenye morali na kila kitu kitakuwa sawa," amesema Mgunda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live