Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgunda: Maandalizi ya kuwavaa KMC yamekamilika

Juma Mgunda Sababu.jpeg Kocha Mgunda.

Fri, 24 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kaimu Kocha Mkuu wa Simba SC, Juma Mgunda amesema maandalizi yote ya kucheza mechi ngumu, nzito yenye kuhitaji matokeo mazuri yamekamilika.

Mgunda amesema hayo leo Mei 24, 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC FC utakaopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Kaluta.

Mgunda ameongeza kuwa ujio wa Simba mkoani Arusha ni nyumbani huku akisisitiza kuwa yeye ni muumini wa mchezaji wa kumi na mbili hivyo amewaomba wawape sapoti kwenye mechi hiyo.

"Kikosi siku hadi siku kinaimarika, mchezaji ambaye nitamkosa katika mchezo wa kesho mchezaji wangu mzuri sana Jobe kwa sababu alipata maumivu mchezo wa juzi, na mtu mwingine ambaye tutamkosa ni Kibu Denis ambaye ameanza mazoezi lakini utimamu wake wa mwili haupo sawasawa," amesema Juma Mgunda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live