Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgoyii, Kizuguto wapewa Mechi ya lawama CAF

Baraka Kizugutooooo Meneja Mashindano TFF, Baraka Kizuguto

Tue, 19 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Ahmed Mgoyi na Meneja Mashindano wa shirikisho hilo, Baraka Kizuguto wamepangwa kusimamia mechi ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Sagrada Esperanca ya Angola na Zamalek ya Misri.

Mgoyi yeye amepangwa na shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) kuwa kamishna wa mechi hiyo huku Kizuguto akipangwa kuwa mratibu wa mchezo.

Mchezo huo utakaochezwa katika Uwanja wa Novemba 11 jijini Luanda, Angola ni muhimu kwa kila upande kupata ushindi kutokana na msimamo wa kundi lao B ulivyo.

Zamalek inayoongoza kundi hilo na pointi tisa, itafuzu hatua ya robo fainali ikiwa itaibuka na ushindi na pia itajiweka katika mazingira mazuri ya kumaliza ikiongoza msimamo.

Timu mwenyeji Sagrada Esperanca inahitajika kupata ushindi ili ifikishe pointi sita ambazo zitaweka hai matumaini yake ya kutinga robo fainali lakini kama ikipoteza, itajiweka pabaya zaidi hasa kama Abu Salim ya Libya iliyo na pointi sita, itashinda ugenini dhidi ya SOAR ya Guinea.

Lakini pia Kizuguto ameteuliwa kuwa kamishna wa mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya Petro Luanda dhidi ya Esperance itakayochezwa kesho Desemba 19.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live