Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgosi: Wachezaji wa Kigeni wanabeba vilabu ila wanaua Timu ya Taifa

Mussa Hassan Mgosi Mussa Hassan Mgosi

Fri, 18 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa zamani wa Simba Queens, Mussa Hassan Mgosi amesema usajili wa wachezaji wa kigeni unakidhi mahitaji ya klabu kuleta ushindani, lakini kwa timu ya taifa inakuwa ngumu.

Akichangia mjadala ulioandaliwa kwenye mtandao wa X na kampuni ya Mwananchi Communications Limited Mgosi amesema inatakiwa kifanyike kitu kwenye timu ya taifa ili iwe na nguvu, akisisitiza wachezaji 12 wanaosajiliwa wanaruhusiwa kucheza wote tofauti na zamani walisajiliwa sita walicheza watatu ambao wazawa walipata nafasi.

Mgosi huo ni mjadala mpana kwasababu unagusa taifa, akishauri kunatakiwa kutafutwe namna ya kuboresha jambo hilo kwa maslahi ya timu ya Stars.

Timu za wanawake ameona wasajiliwa wachezaji wa kigeni angalau watano, watatu wacheze, wawili wasubili ili kulijengea nguvu soka hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live