Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgogoro wa Kimaslahi waivuruga La Liga

G4LpRqUEaNsK G4LpRqUEaNsK Qt6QkwTw8DQZ Original 1440x904 La Liga kuburuzwa Kortini

Wed, 15 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

La Liga kupelekwa mahakamani na vilabu vyake vikubwa ambavyo ni Real Madrid, Barcelona na Athletic Bilbao kutokana na uwekazaji wa Pauni bilioni 1.7 ambao chama cha mpira wa miguu nchini Hispania wameukubali.

Chama cha soka Hispania wiki iliyopita walikubaliana na kampuni binafsi ya CVC Capital Partners ambao watakuwa wanasimamia mapato yote ya hatimiliki ya urushwaji wa matangazo na udhamini wa La Liga.

Siku ya Ijumaa klabu 37 kati ya 42 kwenye ligi kubwa mbili walipiga kura ya kuukubali udhamini huo kutoka CVC Capital Partners, Real Madrid, Barcelona na Athletic Bilbao wamepanga kutoukubali huo udhamini na tayari wanapanga kwende kupinga udhamini huo.

Real Madrid, Barcelona na Athletic Bilbao wameukataa udhamini wa CVC Capital Partners ambao wanadhamani rugby’s Six Nations na awali walikuwa wanahatimiliki ya udhamini Formula 1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live