Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mghana wa Tabora avunja ukimya

Mghana Kitayosce Mghana wa Tabora avunja ukimya

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Straika wa Tabora United, Erick Okutu amesema licha ya kiwango alichoonesha hadi sasa lakini hafurahishwi na matokeo waliyo-nayo akiwatoa hofu mashabiki kuwa timu hiyo haishuki daraja.

Tabora United inashiriki Ligi Kuu kwa mara ya kwanza na haijawa na mwenendo mzuri ikiwa nafasi ya 13 kwa pointi 21 ambapo kwa sasa inaendelea na mazoezi huko mjini Tabora.

Kwa sasa ligi hiyo imesimama kwa muda kupi-sha kalenda ya Fifa, hadi itakaporejea mwezi ujao na timu hiyo itakuwa kibaruani Aprili 14 kuikabili JKT Tanzania.

Okutu, raia wa Ghana tayari amekuwa na ki-wango bora akiwa na uhakika wa namba kikosini na kuwa tegemeo kwenye eneo la ushambuliaji akiwa ametupia mabao saba na asisti mbili katika Ligi Kuu.

Mghana huyo aliliambia Mwanaspoti kuwa licha ya upepo wa Tanzania kumkubali lakini anaumia kuona chama lake halipati matokeo mazuri licha ya wachezaji kujituma kutimiza wajibu.

Alisema wanaendelea kusahihisha makosa yao katika kipindi hiki cha likizo ili warudi na kasi mpya ya kuinusuru timu kushuka daraja.

“Ndio maana tumebaki kambini kuendelea na mazoezi ili kusahihisha makosa yali-yojitokeza yakiwamo binafsi na ya timu kwa ujumla, naamini tutarejea vyema na kuji-nusuru kushuka daraja,” alisema nyota huyo.

Kuhusu vita ya ufungaji bora, nyota huyo alisema bado ni mapema na upinzani ni mkali akieleza kuwa waliomtangulia anapaswa kwenda nao kwa kasi kuhakikisha kila anapo-pata nafasi anafunga bao. Vinara wa mabao ni Stephane Aziz Ki wa Yanga na Feisal Salum ‘Fei Toto’ wa Azam FC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live