Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mghana hashikiki kwa ufungaji Ligi Kuu Z'Bar

Mghana Zanzibar Mghana hashikiki kwa ufungaji Ligi Kuu Z'Bar

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Ligi Kuu ya Zanzibar (ZPL) ipo raundi ya 10 kwa sasa, huku vita ya ufungaji mabao ikizidi kupamba moto kwa nyota wa KMKM, Ibrahim Is-haka akiongoza orodha akiwa na mabao sita.

Nyota huyo raia wa Ghana anafuatiwa kwa karibu na wachezaji watatu wenye mabao matano kila mmoja, huku mabao yake yakiifanya KMKM kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo yenye timu 16 ikikusanya pointi 17 kupitia mechi 10.

Mabao yake yamemfanya Is-haka kuchangia theluthi moja ya mabao ya timu hiyo iliyofunga 16 hadi sasa na kufungwa matano.

Nyota huyo anafuatiwa kwa karibu na Suleiman Mwalimu wa (KVZ), Ibrahim Hamad 'Hilika' wa Zimamoto na Ramadhan Amri Mponda wa Malindi waliofunga mabao matano kila mmoja.

Nyota hao watatu wanafutiwa na wachezaji watatu wenye mabao manne kila mmoja, akiwamo Arqam Ahmed Zubeir wa Kipanga, Ali Khatib Juma wa Uhamiaji na Gamba Idd Matiko wa JKU ambaye jioni yupo uwanjani timu yake ikivaana na Mlandege.

Wachezaji saba wa timu tofauti wanafuata kwenye orodha kila mmoja akifunga mabao matatu, huku wakali wengine 11 nao kila mmoja akifunga mabao mawili.

Katika vita hiyo ya mabao, pia ina jumla ya wachezaji 65 wakifuata kwa kutupia kambani bao moja moja na wachezaji wawili, Abdulkarim Shani Abdallah wa Ngome na Kassim Hassan wa Kipanga wakijifunga wenyewe kwenye harakati za kuokoa mpira kwenye mechi zao dhidi ya KMKM na KVZ.

Wakati JKU ikiwa kileleni mwa msimamo eneo la mkiani wageni wa ligi hiyo Ngome na New City zikiwa mkiani zikikusanya kila mmoja sita tu katika mechi tisa ilizocheza kabla ya mechi za jioni ya leo.

Chanzo: Mwanaspoti