Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mghana Singida FG akumbushia deni lake

Mghana Singidaaaaaaa Nicholas Gyan

Fri, 7 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya kurudi kuitumikia Singida Fountaine Gate huku akiwa ameifungulia madai kwa Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA), nyota kiraka raia wa Ghana, Nicholas Gyan ameuomba uongozi wa timu hiyo kumlipa deni analowadai ili mambo yasiwe mengi.

Gyan alirudishwa Singida baada ya FIFA, kuipa siku 45 timu hiyo kumlipa deni la ada ya usajili huku malimbikizo ya mishahara wakiwa wamefanikiwa kuyatatua.

Akizungumza na Mwanaspoti, Gyan alisema anaidai timu hiyo Sh 50 Milioni ambazo ni malimbikizo ya usajili wa kujiunga na timu hiyo iliyokuwa ni Sh100 milioni walimpa nusu hadi sasa hawajamkamilishia.

“Ligi imeisha na mimi bado nipo Tanzania sijarudi nyumbani nasubiri fedha yangu niliongea na viongozi walikubali kunilipa lakini naona wananiambia niondoke watanilipa nikiwa kwetu,” alisema Gyan na kuongeza;

“Siwezi kuondoka bila hiyo fedha kwani mkataba wa hilo deni umeisha natakiwa kulipwa kiasi changu chote ili niweze kutafuta maisha mengine nje ya Singida Fountain Gate.”

Mwanaspoti lilipojaribu kuwatafuta viongozi wa juu wa timu hiyo simu zao ziliita bila kupokelewa, Ofisa Habari wa SFG, Joseph Mkoko alisema migogoro yote kuhusu timu hiyo na wachezaji watatolea ufafanuzi hivi karibuni.

“Msimu ndio umeisha hivi karibuni mambo ni mengi yamepita hapo katikati viongozi wa juu watakaa na kufanyia kazi changamoto zote na muda ukifika ufafanuzi utatolewa kwa taarifa maalum ya timu,” alisema.

Chanzo: Mwanaspoti