Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgeveke aukubali muziki wa Mayele

Yanga Mayele Ht.jpeg Mgeveke aukubali muziki wa Mayele

Fri, 25 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kitasa wa Dodoma Jiji, Joram Mgeveke ambaye alikuwa akikabiliana na nyota wa Yanga, Fiston Mayele kwenye mchezo wa ligi ambao ulizikutanisha timu hizo, ameukubali uwezo wa mshambuliaji huyo.

Akizungumza na Mwanaspoti mjini hapa, Mgeveke alisema Mayele ni kati ya washambuliaji hatari ambao aliwahi kukabiliana nao kwa ligi na inahitaji akili ya ziada ili kumdhibiti vinginevyo muda wowote anaweza kukuadhibu.

"Jamaa anaweza, sisi tulijiandaa kukabiliana na Yanga na sio Mayele pekee, tulipambana na kila ambaye alikuwa akijaribu kufunga maana mnaweza kusema mdili na mchezaji fulani halafu mkafungwa na mwingine,"

"Matokeo haya yametuumiza lakini naamini yametuachia somo na tutarejea tukiwa bora zaidi kwenye mchezo wetu ujao," alisema.

Beki huyo wa zamani wa Mwadui ya Shinyanga aliwahi kumdhibiti na akashindwa kufurukuta mshambuliaji wa Kinyarwanda, Meddie Kagere kipindi hicho akiwa kwenye ubora wake na Simba kabla ya kutua Singida BS.

Upande wake kocha wa Dodoma Jiji, Melis Medo amepanga kufanyia kazi mapungufu ambayo yalijitokeza dhidi ya Yanga ili kufanya vizuri kwenye michezo yao ijayo. "Tulifanya makosa ambayo yametugharimu, tunatakiwa kuimarika na nafasi hiyo tunayo kutokana na aina ya wachezaji waliopo kwenye kikosi changu," alisema kocha huyo.

UNAHODHA WA MAYELE

Wenye Yanga yao Singida wamechekelea kitendo cha mshambuliaji wao hatari, Fiston Mayele kuvaa kitambaa cha unahodha kwa mara ya kwanza kwa kusema freshi tu kama mbeleni atapewa majukumu hayo moja kwa moja.

Mayele alivaa kitambaa hicho, juzi Jumanne kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji kwenye uwanja Liti, Singida.

Mzee Moyo ambaye ni mmoja wa mashabiki maarufu wa Yanga maeneo ya Msisi na Kititimo alisema kumtishwa Mayele jukumu hilo inaweza kutumika kama sehemu ya kumbakisha klabuni hapi kwa muda mrefu.

Moyo alisema mawazo ya Mayele kuondoka yanaweza kufutika kutokana na namna ambavyo klabu imeamua kumthamini.

"Kuna muda pesa huwa sio kila kitu, mapenzi yetu mashabiki wa Yanga ni kubwa, amekuwa akitufanya tutembee kifua mbele," alisema.

Aisha Majaliwa alisema: "Mayele anapendeza kuwa kapteni maana amekuwa akitupa raha mashabiki wa Yanga."

Mayele alifunga bao la pili akiwa na kitambaa cha unahodha ambacho wakati mchezo ukianza kilivaliwa na Mwamnyeto ambaye alipata majeraha na kushindwa kumaliza dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Chanzo: Mwanaspoti