Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfungaji Bora AFCON afungiwa na FIFA

Nsue Mfungaji Bora Emiliano Nsue

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la soka duniani (FIFA) limemfungia kucheza soka la kimtaifa miezi 6 aliyekuwa mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Guinea ya Ikweta baada ya kugundua kuwa hakuwahi kustahili kisheria kuitumikia timu hiyo ya Taifa kwa miaka yote 11 aliyitumikia.

Baada ya uchunguzi FIFA imeamua kwamba mshambuliaji huyo wa zamani wa Middlesbrough na Birmingham City, Emilio Nsue, hajawahi kustahiki kuichezea Guinea ya Ikweta kwa kipindi chote cha miaka 11 ya maisha yake ya kimataifa kwasababu za utaifa huku pia akiwa ametumikia timu ya Taifa ya Hispania kwa ngazi zote za vijana hadi kufikia umri wa miaka 21.

Licha ya uchunguzi uliowahi kuhitimishwa Desemba 2013 na kugundulika kwa mapungufu kadhaa yanayompa uhalali wa kuchezea Guinea, Nsue aliendelea kuichezea Guinea ya Ikweta, akifunga mabao 23 katika michezo 43 na hivi majuzi alishinda kiatu cha dhahabu kwenye AFCON mnamo Januari .

Kutokana na kasoro hizo, timu yake ya Taifa, Equatorial Guinea wamepokonywa ushindi wao wa kufuzu Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Namibia na Liberia, ambao wote walishinda 1-0 shukrani kwa bao la Nsue.

FIFA imemfungia Emilio kutojihusisha na soka la kimataifa kwa miezi sita, huku shirikisho la Equato Guinean (Feguifut) likipigwa faini ya pauni 129,000.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live