Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfumo wamuondoa Msuva JS Kabylie

Msuva JS Kabylie Simon Msuva

Wed, 20 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Rasmi klabu ya JS Kabylie ya Algeria imechana na mshambuliaji Mtanzania Simon Msuva.

Katika taarifa yake Kabylie mbali na Msuva pia imeacha na mshambuliaji mwingine mkongwe Hichem Mokhtar raia wa Taifa hilo.

Msuva aliyejiunga na klabu hiyo Agosti 27,2023 akitokea Al - Qadsiah ya Saudi Arabia hakufanikiwa kuwa mwanzo mzuti ndani ya timu hiyo kwa kukosa kuanza kwenye mechi nyingi na Waalgeria hao.

Ujio wa kocha Mreno Lui Almeida umechangia kwa kiasi kikubwa kuondoka kwa Msuva ndani ya Kybalie baada ya kocha huyo kushindwa kukubaliana na uwezo wa mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga.

Almeida amewaambia mabosi wa Kabylie kuwa anataka washambuliaji wengine wawili wenye makali zaidi tofauti na hawa ambao a emewatema.

Inaelezwa kocha huyo amewapendekeza wachezaji wawili kutoka Ureno akitaka wasajiliwe na Kabylie haraka.

Chanzo: Mwanaspoti