Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfaransa Tabora aanza mikwara

Dennis Lawrence Taboraaa Kocha mpya wa Tabora United Denis Laurence

Mon, 1 Apr 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati Singida Fountain Gate iliyo chini ya Jamhuri Kihwelo 'Julio' ikiendelea kujifua ufukweni jijini Dar es Salaam, Kocha Mkuu wa Tabora United, Denis Goavec amewatumia salamu akiwatisha amepata kikosi cha maangamizi na kilichobaki ni kupata ushindi katika mechi yao ya ASFC.

Timu hizo zitanatarajiwa kuvaana Aprili 4 katika pambano la hatua ya 16 Bora kwenye Uwanja CCM Kirumba, jijini Mwanza na mshindi wa mchezo huo atafuzu kwenda robo fainali.

Kocha huyo Mfaransa alisema kwa siku saba alizofanya mazoezi akiwa na Masoud Djuma wameridhishwa na viwango vya wachezaji wake na tayari wameshapata kikosi cha kwanza.

Alisema Tabora imesheheni vipaji na kilichobaki ni kutengeneza muunganiko wa vipaji hivyo vilete ushindi, huku akisisitiza mchezaji yeyote atakayemridhisha mazoezini na kufuata maelekezo atapata namba kikosini.

“Katika wiki yangu ya kwanza hapa nimeona maajabu nimesikia raha kuona niko hapa nafurahishwa na wachezaji wananisikiliza na wanafuata kile tunachowataka wafanye manake sijapata shida tangu nimeanza kuwa nao,” alisema Goavec na kuongeza;

“Wana vipaji kama kawaida ya wachezaji wa Afrika, lililopo mbele yetu ni kuviweka pamoja hivyo vipaji wafanye timu ishinde. Tumepata kikosi cha kwanza na tupo tayari kwa mechi zilizopo mbele yetu."

Ofisa Habari wa Tabora United, Christina Mwagala, alisema maendeleo mazuri ya kikosi chao chini ya kocha huyo mpya ni ishara njema kwenye michezo tisa ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho kwani wanahitaji ushindi katika mechi hizo ili kujiweka katika nafasi nzuri.

Chanzo: Mwanaspoti