Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfahamu mchezaji muongo kuwahi kutokea Duniani

Carlos Henrique Raposo Mfahamu mchezaji muongo kuwahi kutokea Duniani

Fri, 17 May 2024 Chanzo: Rasoul HK

Kwa majina Anaitwa 'Carlos Henrique Raposo' maarufu kama Carlos Kaiser, alizaliwa tarehe 2 Aprili mwaka 1963 akiwa mchezaji kutoka Brazil.

Aliwaaminisha watu kuwa yeye anacheza nafasi ya ushambuliaji (Striker). Huyu baharia alidanganya watu na Kuwaaminisha kwamba yeye anajua boli sana na uongo huo aliishi nao Kwa takribani miaka zaidi ya 20.

Carlos alifanikiwa kujiunga na vilabu 12 tofauti tofauti akinasibu kiwa ni mshambuliaji matata wa muda wote.

Katika historia Carlos anafahamika kama mshambuliaji ambaye hakuwahi kupata goli hata moja katika Career yake ya miaka 20.

Uongo wake na utapeli wake wa hali ya juu alikua anaufanya hivi. Mwamba alikuwa anatafuta klabu na kuwashawishi viongozi wa klabu kuwa yeye ni striker

mzuri tuu, na akikubaliwa basi alikuwa anatia saini mikataba mifupi mifupi ila wakati wa mechi lazima alete sababu au afanye tukio ili akwepe kucheza.

Mara nyingi alisingizia kuumia hasa akiwa mazoezini aligiza kupata majeraha ili kukwepa

mechi.

Carlos hakuwai kucheza mechi yoyote katika ile katika career yake hata kwa dakika 5 uwanjani! Lakini kutokana Na njama zake, mwamba alikua anaingiza pesa ndefu mnooo.

Hizo Ndio klabu alizowahi kusaini bila hata kuingia uwanjani au kucheza mechi yeyote.

~Alisaini mwaka 1972 Ndani ya klabu ya Botafogo.

~Alisaini mwaka 1973-1977 katika klabu ya Flamengo.

~Alisaini mwaka 1979-ndani ya klabu ya Puebla.

~Alisaini mwaka 1981 ndani ya klabu ya Botafogo.

~Alisaini mwaka 1983 ndani ya klabu ya Flamengo.

~Alisaini mwaka wa 1986-1987 ndani ya klabu ya Gazélec Ajaccio.

~Alisaini mwaka 1988_ klabu ya Bangu 1988_Fluminense.

~Alisaini mwaka 1989_ ndani ya klabu ya Vasco da Gama.

~Alisaini mwaka 1990_ndani ya klabu ya América (RJ).

~Alisaini mwaka wa 1992 ndani ya klabu ya Guarany Futebol Clube.

Huyu ndiye mchezaji aliyewaaminisha wapenzi wa

soka kua yeye ni striker mkubwa japokua hajui chochote kuhusu soka.

Chanzo : Rasoul HK

Chanzo: Rasoul HK