Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfahamu gwiji Pwele, mfalme wa soka wa Dunia alivyojipatia umaarufu

Peleeeeeee Mfahamu gwiji Pwele, mfalme wa soka wa Dunia alivyojipatia umaarufu

Tue, 6 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Huku basi la timu ya Brazil likipita katika mitaa ya Mexico City likielekea kwenye Uwanja wa Azteca kwa fainali ya Kombe la Dunia la 1970, wachezaji waliokuwemo walionekana wakicheza muziki wa samba kwa furaha.

Kila sehemu inayopatikana, iwe dirisha lililonyeshewa na mvua, paa au kiti kisichotumika, kiligeuka na kuwa chombo cha muziki.

Anayeongoza ngoma hiyo ni winga mwimbaji Jairzinho, 'The Hurricane', mfungaji wa bao katika kila mechi kati ya mechi tano za timu yake kwenye michuano hiyo, zote zikiwa za ushindi.

Anayejiunga ni Roberto Rivellino, kiungo mshambuliaji na mfungaji wa bao la kwanza kati ya 15 lililowapeleka fainali; Carlos Alberto Torres, nahodha mwenye nia thabiti na mahiri ambaye alisaidia kuwazuia mabingwa watetezi England katika hatua ya makundi; Gerson, Tostao, Clodoaldo na wengine, magwiji wa upande huu usio na kifani, wakiwa njiani kuelekea uwanjani.

Kelele ni nyingi mno kwa kila mtu kusikia njuga moja ikianguka sakafuni, wachezaji pia wakijishughulisha na uimbaji wao wakimsifu nyota wao .

Pele - mchezaji maarufu zaidi ulimwenguni, ambaye ameinama akijificha huku machozi yakimtiririk usoni mwake.

………………………

Edson Arantes do Nascimento, anayejulikana kwa ulimwengu kama Pele, alijua mafanikio pekee katika miaka minane ya kwanza ya uchezaji wake wa kimataifa.

Alikuwa na umri wa miaka 16 tu alipoifungia Brazil bao la kwanza mwaka wa 1957, dhidi ya Argentina. Katika muda wa chini ya mwaka mmoja, alifunga mabao mawili kwenye fainali dhidi ya wenyeji Sweden huku nchi yake ikishinda Kombe lao la kwanza la Dunia.

Miaka minne baadaye, huko Chile, jeraha lingepunguza muda wake wa kucheza lakini sio sifa zake wakati Brazil walifanikiwa kuandikisha ushindi mfululizo katika michuano hiyo mikubwa zaidi duniani.

Wakati huo bila shaka alikuwa mwanasoka bora zaidi wa Dunia – mwenye kasi, nguvu, ustadi, akili,na asiye na ubinafsi. Alikuwa nyota wa kimataifa, ambaye umati wa watu ungemiminika kumwona. Aliupenda mchezo huo na ulimsujudia.

Umaarufu kama huo unapatikana kwa gharama. Ilimfanya kukabwa sana katika mechi na katika majira ya joto ya 1966 , wengine hawangeweza kumvumilia.. Ilikuwa katika uwanja wa Goodison Park, nyumbani kwa Klabu ya Soka ya Everton, ambapo mapenzi yake mengi kwa mchezo huo yalipungua.

Beki wa Ureno Joao Morais aalipatiwa jukumu la kumkabili Pele kwa njia yoyote kwenye Kombe hilo la Dunia, kitendo chake cha kikatili zaidi ilikuwa kumkabili mchezaji huyo kwa miguu miwili, safari aambayo ilimwacha fowadi huyo wa Kibrazil akiwa hana uwezo wa kushawishi kile ambacho kingetokea, hatua ilioifanya Brazil kupoteza kwa 3-1.

Matokeo hayo yalithibitisha kutolewa kwa Brazil katika hatua ya makundi na hivyo kuhitimisha umiliki wao wa kujivunia wa miaka minane wa kombe la Jules Rimet .

"Kushindwa kwa aibu" ilikuwa jinsi Pele alivyoelezea baadaye katika wasifu wake, na kuongeza: "Kila mtu alifikiri tungeshinda kwa urahisi. Lakini maandalizi yetu hayakupangwa kwa unyenyekevu sawa na 1958 au 1962. Tayari tulikuwa tunaanza kupoteza taji kabla hata hatujatia mguu Uingereza."

Kwa kupigwa, kujeruhiwa na kukatishwa tamaa kabisa, aliupa kisogo mchezo wa kimataifa.

…………………………

Ilikuwa pigo kwa Brazil. Nguvu za Pele zilizidi uwezo wake kwenye uwanja wa mpira. Alikuwa nguvu ya kuunganisha nchi kubwa na zenye tamaduni nyingi na maeneo makubwa masikini, ambayo yeye mwenyewe alitoka. Alikuwa ishara ya matumaini.

Huyu alikuwa mtu ambaye aliwahi kutangazwa "hazina ya kitaifa isiyoweza kuuzwa nje" kufuatia kikao cha dharura cha Congress wakati vilabu kutoka Italia vilikuja kuwinda saini yake katika ujana wake.

Umuhimu wake kama kiongozi uliongezeka tu wakati wa ukosefu wa utulivu na kutokuwa na uhakika, na nchi chini ya utawala wa kijeshi kufuatia mapinduzi ya 1964.

Kuachilia mbali Kombe la Dunia lilikuwa pigo. Kumpoteza Pele ilikuwa jambo lisilofikirika.

Muda unaweza kuwa mponyaji mkubwa, kama vile mtazamo unavyoweza. Pele alipata faraja katika miaka michache iliyofuata na mawazo yalipoanza tena kuelekea Kombe la Dunia alikuwa mtu aliyebadilika na kuwa mtu aliyeasitisha uzoefu wake nchini Uingereza.

Uzazi ulisaidia kupunguza hali ya kutoridhika kwake na soka, wakati alipotembelea Afrika na Santos na kushuhudia umati mkubwa wa watu wenye shauku waliokusanyika kumwona mtu mweusi na upande wake ulimpa mtazamo mpya juu ya umuhimu wake kama mfano wa kuigwa.

Pia alikuwa akijawa na imani mpya baada ya misimu kadhaa ya klabu, ambapo alifikisha lengo lake la uchezaji hadi kufikia magoli 1,000 wakati muhimu zaidi nchini Brazil, ambapo habari za mtu huyo kufikia kiwango hicho zilitangazwa katika ukurasa wa kwanza wa magazeti pamoja na zile za watu 12 kutua katika mwezi.

Pele pia hakuwa salama kutokana na hofu kubwa kwa nyota wote wa michezo ya kutaka "kutomaliza uchezaji wao kama mtu aliyeshindwa".

Hatimaye baada ya kushawishika kurejea katika kikosi cha timu ya taifa kwa ahadi za Tume ya Michezo ya Brazil kuimarisha maandalizi na kuzuwia mchezo mchafu kupitia kuanzishwa kwa kadi za njano na nyekundu kwenye michuano hiyo nchini Mexico, uamuzi wa Pele ulithibitishwa na kufuzu katika kampeni.

Alichangia mabao sita kati ya 23 yaliyofungwa , timu ya Brazil iliyochangamka ilipata ushindi wa mechi sita kati ya sita chini ya kocha Joao Saldanha.

Hatahivyo, utulivu uliokuwepo ulibadilika na kusababisha magogoro, huku kocha Saldanha akihusika na msukosuko huo, akionekana kudhamiria kutengua kazi yote nzuri kwa kugongana na vyombo vya habari, akitumia mikakati mibovu wakati Brazil iliposhindwa na Argentina – huku akihoji kwa dharua nafasi ya Pele.

Mgogoro wake mkubwa zaidi ulikuwa kati yake na Jenerali Emilio Garrastazu Medici, rais wa utawala wa kijeshi wa Brazili, ambaye hakupenda kuambiwa ajiepushe na masuala ya timu ya taifa.

Saldanha alifukuzwa kazi muda mfupi baadaye, lakini alikataa kwenda kimya kimya, akidai sehemu moja ya matokoe yake mabaya ilikuwa mchezaji nambari 10, kwanza akisema kwamba alikuwa na haoni mbali (jambo ambalo lilikuwa la kweli kiufundi lakini lilikuwa jambo ambalo halikudhuru mchezo wake }Vilevile alimlimbikizia lawama mchezaji huyo akidai kwamba alikuwa hafai na anaugua "ugonjwa mbaya", na kumfanya Pele aliyekuwa na wasiwasi kupata uhakikisho kutoka kwa madaktari wa timu.

Ingawa Pele hakuwa na wasiwasi wowote uwanjani, lilikuwa jambo tofauti.

Alikuwa maarufu huko Mexico. Ziara moja ya Guadalajara pamoja na timu ya Brazili ilisababisha karibu mji mzima kufungwa, huku mabango yakiwa yamewekwa kwenye kona za barabara yakisema: "Hakuna kazi leo, tumeenda kumwona Pele!"

Lakini nchi hiyo ilikuwa na hali tete ya kisiasa katika majira ya kiangazi ya 1970. Kukamatwa kwa kundi la wapiganaji wa msituni waliofunzwa kutoka Cuba na polisi kulipelekea taarifa ya njama inayoweza kumteka nyara nyota huyo wa Brazil kabla ya Kombe la Dunia.

Kutokana na hali hiyo, katika wiki chache kabla ya michuano hiyo, Brazil ilifanya mazoezi katika kambi yenye ulinzi wa usiku na mchana ikilindwa na polisi na walinzi wenye silaha, huku Pele mwenyewe akiwa amejificha nyuma ya duara la ulinzi popote alipokwenda.

Ilipofika, mchezo wao wa kwanza dhidi ya Czechoslovakia katika uwanja wa Estadio Jalisco ulikuwa wa kujitolea , sio tu kwa Pele bali kikosi kilichokuwa makini, kilichoboreshwa na watu milioni 96 waliotazama mechi hiyo yumbani kutoka Brazil.

Mexico 1970 ilikuwa mlipuko wa rangi, na hakuna upande ulikuwa na mchanganyiko wa rangi zenye utajiri kuliko Brazil.

Katika shindano lililopeperushwa moja kwa moja na kwa teknolojia kamili kwa mara ya kwanza kwa hadhira ya kimataifa ambayo mwaka mmoja tu uliopita ilikuwa imemshuhudia Neil Armstrong akitua kwenye mwezi, mwendo wa mpira na ustadi wa hali ya juu wa wale waliovalia rangi ya manjano ya canary na buluu ya kobalti ulikuwa mzuri katika ulimwengu mpya wa mpira wa kijasiri na mzuri.

Wakiwa wamepewa uwezo wa kutumia uhuru wao na akili pamoja na uwezo wao na mrithi wa Saldanha Mario Zagallo, mchezaji mwenza wa zamani wa Pele miaka ya '58 na '62, wao ulikuwa mchezo wa kushambulia.

Wakiwa wamebarikiwa na idadi kubwa ya wachezaji 10, Zagallo alipata njia ya kuwashughulikia wote - Jairzinho na Rivellino wakifanya kazi nyingi tofauti, Tostao kama tisa wa uongo na Gerson akicheza zaidi katika safu ya kiungo.

Katikati ya wote alikuwa Pele, sumaku ya mpira uwanjani na mboni za macho nje yake, kila mguso wake ulikuwa wa maana, mbio zake za mbele zikichemka kwa nia na matumaini.

Mchezo wake ulikuwa ukizingatia udhibiti, kasi, nguvu na maono, lakini hapa viliunganishwa kwa upatanishi kamili na mabadiliko yake kama mchezaji.

Mwaka '58 alikuwa mbichi, mwaka '62 alijeruhiwa, mwaka'66 aliathiriwa lakini mwaka 1970 alikuwa mzoefu, fiti, huru na makini. Huyu alikuwa Pele asiye na kasoro, asiye na dosari na aling'aa kuliko hapo awali.

Mchezo wa ufunguzi ulikuwa pingamizi kali kwa wale wote ambao walikuwa wamemkataa, ikiwa ni pamoja na kocha wa Czech Jozef Marko ambaye timu yake ilichukua uongozi wa mapema lakini alipata mshangao mkubwa na kumuelezea kwa hasira nyota huyo "nguvu iliyotumika".

Mabao mawili ya Jairzinho ya dakika za lala salama yalikamilisha kipigo cha 4-1.

Kile ambacho wengi wanakumbuka zaidi kwenye mchezo huo, halikuwa bao Pele alilofunga, lakini lile ambalo hakufunga akiwa katika upande wa goli lake na kujaribu kungua kipa wa timu ya pinzani kwa kuuinua mpira uliompita kipa wa Czech Ivo Viktor lakini ukatoka nje kwa inchi chache.

Jairzinho aliifungia Brazil bao la ushindi lakini lilitokana na ustadi wa Tostao, ambaye aliwachenga mabeki watatu wa England kabla ya kupiga krosi, ambayo iliguswa na Pele aliyempigia pasi mfungaji huyo.

"Brazili ilipofunga bao lao la ushindi, tuliona kipengele kingine muhimu cha mchezo wa Pele unyenyekevu, "Pele aliwakata mabeki wawili wa Uingereza kabla ya kumpitia pasi rahisi Jairzinho aliyecheka na wavu. Huyo alikuwa Pele kwa umahiri wake.

"Uchezaji wake huko Mexico hakika ulionyesha ubora wake uliona talanta ambayo alikuwa ameiboresha hadi kufikia mahitaji yote muhimu ya kushinda mechi. Ikiwa pasi rahisi ingefaa zaidi kwa timu, angeicheza. Alikuwa injini na moyo wa Brazil, na pia kuwa mfano bora wa hisia bora za taifa hilo kwa mchezo."

Nahodha wa Uingereza Bobby Moore, mtu ambaye alinyanyua kombe la Jules Rimet miaka minne iliyopita, alimpongeza Pele kwa muda wote, akibadilishana mashati naye, na hivyo kukumbatiana bila wasiwasi.

Ushindi wa 3-2 dhidi ya Romania huku Pele akifunga mara mbili kupitia mkwaju mkali wa faulo na, umaliziaji wa chinichini - uliwafanya wawe kileleni mwa kundi na kuanzisha sare ya mtoano na Peru.

Ingekuwa robo fainali kwa zama zilizopita, mechi ya wapinzani wa Amerika Kusini wenye nia moja, wakishambuliana moto kwa moto.

Waperu hao walikuwa na fursa ya mchezaji wa ndani katika usukani wa Didi, mchezaji mwenza wa zamani wa Pele kwenye Kombe la Dunia la '58 na '62. Hatimaye, Wabrazil waliibuka washindi, wakishinda 4-2 katika mechi ambayo ilisisitiza zaidi umoja wao.

Hii ilikuwa Brazil iliyounganishwa, familia. Nje ya uwanja ibada ya usiku ilikuwa imeanza, ikiongozwa na Pele Mkatoliki.

Wachezaji wangekusanyika pamoja kuombea kwa ajili ya wagonjwa, maskini, wahasiriwa wa vita vinavyoendelea Vietnam, lakini sio kuombea ushindi, kwani hilo walipaswa kupata. Ili kufanya hivyo, wangelazimika kumuua roho mwovu wa kale.

Pele alikuwa na umri wa miaka tisa wakati Brazil iliposhindwa na Uruguay - mmoja wa wapinzani wao wa jadi - katika fainali ya Kombe la Dunia la 1950 kwenye ardhi ya nyumbani.

Siku ambayo ilikuwa imeanza kama siku ya matumaini na furaha – huku ikijaa sauti za fataki na sauti za juu za redio - iliishia kwa kukata tamaa na kimya.

Akirudi nyumbani kutoka kwa mchezo wake mtaani, ambapo alicheza kwa kutumia mpira uliofungwa na makaratasi na kamba, Pele alimkuta baba yake akitokwa na machozi.

Dondinho, mwanasoka mwenye kipawa cha hali ya juu , alikuza upendo was oka kwa mtoto wake akimpatia mbinu na hekima. Sasa mwana alipata fursa ya kutoa kitu kama malipo.

Katika chumba cha baba yake, alitazama picha ya Yesu ukutani. "Kama ningekuwa huko nisingeiruhusu Brazil kushindwa," alisema. "Kama ningekuwa huko Brazil ingeshinda." Miaka ishirini baadaye, alitimiza ahadi hiyo.

Mechi haikuanza vizuri. Uruguay iliongoza nusu fainali mjini Guadalajara baada ya dakika 20. Hata hivyo, katikati ya kipindi cha kwanza, Brazil walianza kutawala na, ikiwa imesalia dakika moja kabla ya mapumziko, Clodoaldo alifunga bao lake la kwanza la kimataifa.

Pele alikuwa kimya lakini ushawishi wake kwenye mchezo uliongezeka na kuongezeka. Alitamba na mpira kushambulia kombora la mara ya kwanza ambalo lilizuiliwa na kipa wa Uruguay , na kombora jingine likaja muda mchache baadaye lakini likatoka nje.

Bao la dakika za mwisho dhidi ya Uruguay, ambao walikuwa wametolewa katika muda wa dakika za ziada na USSR katika hatua ya nane bora, lilikuja wakati Jairzinho alipopokea pasi kutoka kwa Pele ikiwa zimesalia dakika 15 mpira kumalizika. Pele asiyechoka alimpigia pasi Rivellino kwa bao la tatu katika hatua za mwisho.

Katika dakika za lala salama, mpira wa Tostao kwa Pele ulimtoa nje kipa wa Uruguay, Ladislao Mazurkiewicz, lakini badala ya kumsogeza mbele fowadi huyo aliduwaa, na kuruhusu mpira kuwapita yeye na mpinzani wake.

Matokeo hayo yalitimiza ahadi ya Pele kwa baba yake na kuiwacha Brazil ikiwa imbakisha mchezo mmoja kushinda taji hilo la dunia.

Huku akitokwa na machozi usoni mwake na mlio wa kujirudia-rudia wa mdundo wa muziki wa samba wa wachezaji wenzake ukijaza masikio yake, Pele anajituliza.

Huu sio wakati wa shaka. Ndiye mchezaji aliyeimarika zaidi kati ya wachezaji wa nchi yake, bingwa wa dunia mara mbili, kiongozi. Akiwa amefunga safari ya kufika hapa, hafai kujikwaa tena.

Anainua sauti yake, anasimama kwa miguu yake tena na kujiunga tena na okestra ya bendi yamuziki wa samba unaopitia mitaa ya Mexico City.

Saa chache baadaye, mpiga picha ananasa picha ya timu za Brazil na Italia zikiwa zimejipanga kwenye Uwanja wa Azteca kabla ya kuanza kwa mchezo huo, mashabiki 100,000 wakiwazomea kutoka pande zote za uwanja uliofurika katika mji mkuu wa Mexico.

Ndani yake, picha ya karibu ya nyuso za wachezaji wa Brazil walio na wasiwasi tayari kwa mechi hiyo ya fainali, isipokuwa Pele, ambaye anatazama upande wake wa kushoto, moja kwa moja chini ya lenzi ya kamera na mwenye mwonekano wa utulivu na kujiamini.

Kwa hatua za ufunguzi, Italia ilicheza mbinu ya Catenaccio inayofunga lango lao. Lakini dakika ya 18 fursa ilipatikana. Msalaba wa Rivellino umenasa na una matumaini, Pele anamkimbia Tarcisio Burgnich, akihakikisha anaruka juu zaidi na kufunga bao sahihi la kichwa.

Pele anaruka tena, safari hii kwenye mikono ya Jairzinho, ngumi yake ikisukuma hewa. Kabla ya mapumziko, wanapata pigo. Mlinzi wa Brazil, Roberto Boninsegna afanya masihara na kujifunga .

Hakuna hofu wakati wa mapumziko. Brazil ndio timu ilioimarika baada ya nusu fainali ya mbio za marathon ya Italia dhidi ya Ujerumani Magharibi siku nne zilizopita. Wana talanta na mpango wa busara kutumia fursa yoyote mbele yao.

Pele yuko inchi kadhaa mbali na krosi ya Carlos Alberto, Rivellino anapiga mpira wa krosi kutoka kwa mpira wa adhabu. Ni dakika ya 66 ambapo Gerson anakusanya mpira pembezoni mwa eneo la goli na kupiga shuti lililopita kushoto mwa Enrico Albertosi na kuingia wavuni.

Muda mfupi baadaye, pasi ya Gerson ya mbele ilikutana na kichwa cha Pele - akiruka kwa mara nyingine nyuma ya Burgnich na kukamilisha kazi kamili ya kufunga katika kila mchezo wa dimba.

Dakika 15 zinazofuata zinapita katika ukungu usio na mvuto, jukwa la mashati ya manjano likicheza kuzunguka adui aliyehuzunika.

Waitaliano wanalilia filimbi ya mwisho wakati Tostao anarejea kushinda mpira na kumwachia Wilson Piazza, ambaye kisha anasaidia kusawazisha.

Kiungo huyo anawachenga wataliano wanne na kumtafuta Rivellino, ambaye anapiga pasi inayompata Jairzinho chini kushoto. Anakata ndani na kumtafuta Pele, ambaye anapiga mpira kwa uzito wa kutosha kwa Carlos Alberto ambaye anapiga mara moja kwenye kona ya mbali ya wavu.

Ni kazi ya sanaa. Ukamilifu. Lengo linaloonyesha yote ambayo Brazili hii inasimamia kazi ya pamoja, ujuzi, uboreshaji, usahihi na kupanga.

Zagallo alikuwa amelitambua Eneo la kushoto la timu ya Itali kama Eneo ambalo lilikuwa na fursa kwa Wabrazil kulitumia, lakini hata yeye hangeweza kufikiria wangefanya hivyo kwa mchezo mzuri kama huo.

Kwa mara nyingine tena katika hatua muhimu kulikuwa na Pele, pasi yake ya ilikuwa sahihi sana na kamili katika utekelezaji wake, kutojitolea kwake hakukuwa `na mfano mwengine.

Wapiga picha walivamia uwanja wakitafuta picha nzuri. Kwa muda wote, mashabiki walimiminika uwanjani kuwakumbatia wachezaji wa Brazil, wakiwararua mashati na kaptula.

Pele ni mmoja kati ya wengi waliotoka uwanjani bila shati, akiwa amelivua mwenyewe ili kuepusha kuumizwa na kucha mgogoni . Anaingia katika chumba cha maandalizi na kuanza kuomba.

Mwandishi wa habari anaingia na kupiga magoti mbele yake kuomba msamaha kwa mashaka kuhusu fowadi huyo ambaye alikuwa amechapisha kabla ya mashindano.

Pele anamkaribisha kwa miguu yake. “Ni Mungu pekee ndiye anayeweza kusamehe,” anamwambia. "Na mimi si Mungu."

Muda fulani baadaye, wakati kivumbi kilipokuwa kimetulia kwa Mexico 1970 na ushujaa wa Pele ulikuwa tayari umeanza kuingia kwenye hadithi, Burgnich - mtu aliyepewa jukumu la kujaribu kumzuia Pele kwenye fainali - aliulizwa kuhusu uzoefu huo.

"Nilijiambia kabla ya mchezo, 'Yeye ameumbwa kwa nyama na damu, kama mimi.'" alitafakari. "Nilikosea."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live