Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfahamu Nickson Kibabage

Kibabage Yts Mfahamu Nickson Kibabage

Mon, 10 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Majina yake kamili anaitwa, Nickson Clement Kibabage, alizaliwa Oktoba 12, 2000 (23). Ni Versatile player, anamudu vema kucheza eneo la full back wa kushoto (3).

Nafasi zingine anazomudu kucheza ni Kwenye eneo la kiungo mkabaji (6),vwinga zote mbili (7,11) na full role (10).

Baada ya kumaliza Elimu yake ya Secondary pale Morogoro Secondary mwaka (2016) alijiunga na Taasisi ya kulea vipaji vya vijana (MORO KIDS) Mkoani Morogoro.

Baadaye alibahatika kuchaguliwa kujiunga kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Vijana (U17) chini ya kocha, Kim Poulsen na Bakari Shime. Baadaye akaitwa timu ya Taifa (U20 & U23).

Alicheza Moro Kids akiwa na Kibwana Shomari, Dickson Job Mshery na wengine, baadaye wakapelekwa katika klabu ya Mtibwa Sugar kwenda kufanya majaribio.

Wote wakafaulu kisha wakasaini mikataba ya kuanza kuitumikia Klabu hiyo. Baada ya kuitumikia Mtibwa akiwa kinda, Kibabage alitolewa kwa mkopo kwendakatika Njombe Mji FC, mkataba ulipoisha akarejea katika klabu ya Mtibwa sugar.

Baada ya kufanya vizuri akiwa Mtibwa Sugar aliitwa nchini Morocco kwenda kufanya majaribio katika klabu ya Diffaa El Jadida na baada ya kufanya vizuri alisajiliwa rasmi kwa mkataba rasmi kuitumikia klabu hiyo mwaka 2019. Alimkuta pia Simon Msuva.

Septemba 2020, Klabu ya Diffaa El Jadida ilimtoa kwa mkopo kwenda katika klabu ya Youssoufia Berrechid. Juni 30, 2021 alirejea Diffaa El Jadida baada ya mkopo wake kumalizika. Kikafuata kipindi cha CORONA akarejea nyumbani Tanzania.

Septemba 5, 2021 alijiunga rasmi na klabu ya KMC wakati akisubiri CORONA ipite. Baadaye ilitangazwa amesajiliwa rasmi baada ya kuvunja mkataba katika klabu ya Diffaa El Jadida kwa makubaliano ya pande mbili.

Agosti 1, 2022 alisajiliwa na klabu ya Mtibwa Sugar, akacheza vizuri klabu ya Singida Big Stars (sasa Singida Fountain Gate) ikamsajili Februari 26, 2023.

Julai 5, 2023 Kibabage alijiunga na Klabu ya Yanga akitokea katika klabu ya Singida Fountain Gate baada ya kufanya vizuri katika muda mfupi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: