Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfahamu Mamadou Doumbia; chuma kipya cha Yanga

Mamadou Doumbia Mamadou Doumbia

Mon, 16 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya wamelamba dume kwelikweli baada ya kumalizana na beki wa kimataifa raia wa Mali, Mamadou Doumbia kwa kuwa nyota huyo ana sifa tano kali ambazo zinatarajiwa kumbeba ndani ya kikosi hicho cha kocha Nasreddine Nabi.

Beki huyo kwa sasa yupo na timu ya taifa ya Mali katika michuano ya CHAN inayoendelea nchini Algeria.

Beki huyo atakuja kuongeza nguvu katika safu ya ulinzi ya Yanga ambayo kwa sasa ipo chini ya mabeki wanne Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Yannick Bangala na Ibrahim Bacca.

Championi limetazama kwa makini safu ya Yanga na kisha kubaini sababu za Yanga kumuongeza Doumbia huku likibaini sifa hizi 5 kutoka kwa beki huyu ndiyo chanzo cha mabosi wa Yanga kumsajili beki huyu.

UREFU

Ukimtazama beki huyu utabaini ni mrefu kuliko mabeki wote wa Yanga waliopo kwa sasa huku akiwa amempita kidogo urefu Mwamnyeto ambaye ndiye mrefu kuliko wote katika safu ya ulinzi ya Yanga.

Yanga walikuwa wanahitaji beki mwingine mrefu ili kuliipa uhai eneo la kujilinda haswa kulingana na mipira ya juu huku wakiamini beki huyo atawasaidia vyema.

KUZUIA MIPIRA YA KICHWA

Tatizo kubwa la Yanga katika michezo ya hivi karibuni limeonekana katika mipira ya krosi na beki huyu ni hodari katika kuzuia mipira ya juu kutokana na urefu wake jambo ambalo kwa Yanga wanaona watakuwa wametibu tatizo kwa kumleta beki huyu.

UZOEFU KIMATAIFA

Doumbia ana uzoefu mkubwa katika michuano ya kimataifa, amekuwa akiitumikia timu ya taifa ya Mali katika michezo mingi kuanzia AFCON na CHAN jambo ambalo Yanga wanaamini kuwa uozefu huo utawasaidia katika michezo yao ya Kombe la Shirikisho Afrika.

UONGOZI

Jamaa ukiachana na kuwa beki mgumu kupitika lakini ni kiongozi kwani amekuwa nahodha msaidizi wa kikosi cha Stade Malien, jambo ambalo litakuwa faida pia kwa Yanga kuwa na viongozi wengi kama Mwamnyeto, Khalid Aucho, Bangala, Job, Djuma Shabani na Fiston Mayele.

MTAALAMU WA PASI NDEFU

Doumbia amekuwa na sifa nyingine nyingi kama vile kuchezesha timu kutokea nyuma kutokana na uwezo wake mkubwa wa kupiga pasi ndefu kwa ufasaha na hiyo itakuwa faida kubwa sana kutokana na wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kukimbia kama Bernard Morrison, Tuisila Kisinda, Jesus Moloko na Mayele.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live