Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfahamu Kocha mwenye umri mdogo zaidi Afrika kutoka Tanzania

Xavi Bongoo Mfahamu Kocha mwenye umri mdogo zaidi Afrika kutoka Tanzania

Wed, 26 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Kijana Mohammed Mrishona Mohammed maarufu kama Kocha Xavi kutoka Tanzania ndiyo Kocha mwenye umri mdogo zaidi kwa sasa hapa Afrika mwenye leseni ya CAF A Diploma.

Mohammed Mohammed (Xavi) ni Kocha Mkuu wa Simba U20 vile vile ni Kocha wa Timu ya Vijana ya Zanzibar kuanzia U15 na U17, mwaka jana alikua Kocha Msaidizi wa Serengeti Girls (U17).

Moja ya mafanikio ya Kocha Xavi ni kuwapa Ubingwa Zanzibar katika Mashindano ya Cecafa Mwaka jana yaliyofanyika Uganda chini ya miaka 15.

Moja ya mchango wake ndani ya Simba U20 ni kuifikisha hatua ya nusu fainali msimu huu huku ikiwachukua Simba SC zaidi ya miaka 4 kufika hiyo na wakati anaichukua ilikua inaburuza mkia “wa mwisho kwenye kundi."

Mwaka 2023 Kocha Xavi aliingia kwenye kinyanganyiro cha kuwania kocha Bora wa mwaka 2023 Tunzo za BMT ila hakufanikiwa kushinda.

Kwa sasa anafanya kazi bora sana haswa kipindi Ligi imesimama ya kuhakikisha Wachezaji wanakua timamu kwa programu maalumu huku akiwa na leseni na cheti Fitness

Nyota wakubwa wa Hapa Nchini wakiwa mapumziko/likizo huungana na kufanya mazoezi maalumu kutoka kwa Kocha Xavi, Nyota hao ni:-

Simon Msuva. Mudathir Yahya Fei Salum. Chrispin Ngushi. Said Junior. Adam Salamba. Eliuter Mpepo Mapinduzi Balama. Edmund John James Msuva. Agrey Malik. Ibrahim Ame. Ibrahim Bacca. Kibwana Shomari. Ayoub Lyanga. Anuar Jabir Ali Msengi. Yohana Mkomola Abdul Aziz Makame “Bui”. Kevin Sabato.

Kwa upande wa Kike. Opah Clement Irine Kisisa. Enekia Kasonga Lunyamila Diana Niyonzima Aisha Masaka Fetty Densa. Mwanahamis Omar “Gaucho”. Clara Luvanga.

Ndani ya muda mfupi Kocha Xavi amefanya makubwa kwenye Soka huku akiendelea kufanya bora kutokana na uwezo na ujuzi wake katika kufundisha/kuipa Utimamu Timu na ufundishaji wake unavutia sana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live