Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfahamu Hafeez Draghi mtangazaji pendwa wa soka Duniani

HAFID DARAJI Hafeez Draghi.

Thu, 9 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Moja ya watangazaji wa soka wenye mashabiki wengi duniani ni Hafeez Draghi raia wa Algeria. Draghi amekuwa maarufu kutokana na aina ya utangazaji wake wa soka.

Mtangazaji huyo wa Kituo cha Bein Sports amekuwa akivutia watazamaji wengi wa mpira ambao hupenda kusikia jinsi anavyotangaza na kutaja majina ya wachezaji.

Draghi jana ndiyo alilitangaza pambano la Nusu Fainali ya Uefa Champions League iliyozikutanisha timu za Real Madrid na Bayern Munich.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Santiago Bernabeu, Madrid walishinda mabao 2-1, huku wakitokea nyuma baada ya kufungwa 0-1 hadi dakika ya 87, lakini mpaka kufikia dakika ya 90 Madrid walikuwa wanaongoza 2-1 na mechi ikaisha hivyo na Madrid kutinga hatua ya Fainali ya Michuano hiyo kwa Agg 4-3.

Madrid watakutana na Borrusia Dortmund June 01,2024 kwenye fainali itakayochezwa kwenye dimba la Wembley Jijini London.

Vipi ushawahi kumuona Draghi akitangaza soka kando ya kuisikia sauti yake tu?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live