Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfahamu Feisal Salum 'Fei Toto'

Feisal Mfahamu Feisal Salum 'Fei Toto'

Wed, 22 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

FEISAL SALUM maarufu kama 'Fei Toto' amezaliwa 11 Januari, 1998 visiwani Zanzibar, alianza maisha yake ya soka kwenye timu ya mtaani kwao inayoitwa Aston Villa kisha akaenda kwenye timu ya Seminary inayoitwa Criss alilelewa hapo kisoka.

Inaelezwa kuwa wazazi wake hawakupenda yeye acheze mpira walipenda asome zaidi na aachane na soka lakini baada kusajiliwa na JKU wazazi wake walishtuka sana na kuona kijana wao ni mchezaj bora hadi anasajiliwa na timu kubwa Zanzibar.

Hapo ndipo wazazi wake walianza kumpa sapoti kubwa katika safari yake ya soka. Feisal alisajiliwa JKU 2016 alihudumu hadi 2018 ambapo alikuwa akicheza kama mshambuliaji namba 10.

Wakati huo alikuwa kijana mdogo lakini hatari asiye na huruma na goli wala kipa kwa mashuti makali mithili ya radi.

Julai 12, 2018, Feisal alitangazwa kusajiliwa na Singida United na akaonekana amesaini mktaba na kupewa jezi, lakini saa chache baadae alitangazwa kuwa amesajiliwa na Yanga.

Jambo hilo liliibua mijadala mingi, mchongo huo ulichezwa na aliyekuwa mfadhiri wa Singida United na shabiki wa Yanga, Mwigulu Nchemba ambaye ndiye alimpeleka Yanga na kuahidi kumlipa mshahara na stahiki zake zote.

Akiwa Yanga, Feisal alianza kupewa majukumu ya kiungo namba 6, kisha kiungo namba 8.

Feisal aliaminiwa zaidi na aliyekuwa Kocha wa Yanga, Papa Mwinyi Zahera na kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Emmanuel Amunike.

Feisal alicheza nafasi tatu tofauti na kuonesha kiwango bora bila kuchuja hata msimu mmoja, na kila siku amekuwa akiongeza ubora tofauti na mwanzo kiasi cha wachambuzi na wadau wa soka kumtaka sasa akacheze nje ya nchi hata Ulaya kutokana na kiwango chake kuwa bora.

Sasa anakiwasha mpaka wapinzani wake wanaomba poo. Kwa msimu huu, Feisal mpaka sasa ndiye kinara wa mabao Yanga akiwa na mabao manne na asisits 2.

Naam huyo ndio Feisal Salum, amecheza mechi 127 akiwa na Wananchi, si rahisi kwa umri wake kucheza mechi nyingi kwa nafasi tofauti akionesha ubora wa hali ya juu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live