Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mexime ajipa matumaini kibarua chake

60978 MAXIME+PIC

Mon, 3 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Mexime amesema hana presha ya kibarua chake kuota nyasi kutokana na mwenendo wa timu yake msimu huu wa Ligi Kuu Bara.

Kagera Sugar ni miongoni mwa timu mbili, ikiwemo Mwadui FC ya Shinyanga ambazo ziko kwenye hatari ya kushuka daraja huku wakiwa na matumaini pekee ya kusalia kupitia michezo ya mchujo.

Mexime alisema kilichotokea msimu huu ni kipindi ambacho kinaweza kuikuta timu yoyote kwa hiyo anachokifanyia kazi zaidi ni kuinasua timu yake.

“Tunaweza kusalia, hilo sina shaka nalo. Tumejiandaa na nina imani kubwa na wachezaji wangu kwa sababu mechi hizi mbili ni kama fainali kwetu,” alisema kocha huyo.

Pamoja na kuwa kwao kwenye hatari ya kushuka daraja, Kagera Sugar ndio timu pekee msimu huu ambayo iliifunga Simba kwenye michezo yote miwili ya ligi hiyo.

Katika hatua ya mchujo wa kusalia Ligi Kuu, Kagera Sugar watacheza na Pamba ya Mwanza leo kwenye uwanja wa Nyamagana huku wenzao Mwadui wakicheza dhidi ya Geita Gold.

Pia Soma

Michezo ya marudiano itakuwa Juni 8 na washindi wa jumla kwenye michezo yote hiyo miwili watakuwa wamesalia au kupanda Ligi Kuu kwa msimu ujao wa 2019/2020.

Hii ni mara ya kwanza kwa mfumo huo kuanza kutumika katika Ligi Kuu Bara.

Chanzo: mwananchi.co.tz