Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mexime aanza kivingine Kagera Sugar

Kagera Pic Mexime Mexime aanza kivingine Kagera Sugar

Tue, 1 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha mpya wa Kagera Sugar, Mecky Mexime leo ataiongoza timu hiyo katika mchezo wake wa kwanza Ligi Kuu dhidi ya KMC muda mfupi ujao kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza tangu alipotangazwa juzi Jumapili kurithi mikoba ya Francis Baraza ambaye mkataba wake umesitishwa.

Mexime ambaye amesaini mkataba utakaomuweka kwa wakata miwa hao hadi mwisho wa msimu huu (Juni 2023) ameanza kazi kwa kupangua kikosi cha mwisho kilichopangwa na Baraza dhidi ya Namungo FC na kuchapwa mabao 2-1.

Katika kikosi hicho, Mexime amewapumzisha nyota wawili Yusuph Dunia na mshambuliaji, Hamis Kiiza ambao sasa wataanzia benchi huku nafasi zao zikichukuliwa na Abdallah Seseme na Meshack Mwmaita.

Mbali na nyota hao wawili, wachezaji wengine tisa walioanza katika mchezo uliopita ambao ulikuwa wa mwisho kwa Kocha Francis Baraza wameanza katika kikosi cha leo dhidi ya KMC.

Kikosi cha Kagera ni; Said Kipao golini mabeki wa pembeni, David Luhende na Datius Peter, mabeki wa kati, Abdallah Mfuko na Laurent Alfred, viungo ni Abdallah Seseme na Appolinaire Ngueko, mawinga ni Yusuph Mhilu na Meshack Mwamita huku mshambuliaji akiwa Mbaraka Yusuph.

Wachezaji wa akiba ni Ramadhan Chalamanda, Mpapi Nasibu, Yusuph Dunia, Erick Mwijage, Hamis Kizza, Deus Bukenya, Abeid Athuman, Ally Ufudu na Anuary Jabir.

Chanzo: Mwanaspoti