Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mexime: Sina neno, Ihefu tumezidiwa na Yanga

Mexime Yanga Mexime: Sina neno, Ihefu tumezidiwa na Yanga

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Soka ya Yanga imeendeleza kasi ya kuwania Ubingwa wa Ligi Kuu Bara kufikisha pointi 49 baada ya kuifunga Ihefu SC magoli 5-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar

Magoli ya Pacome Zouzoua (10) na Mudhathir Yahya (30) Aziz Ki (68), Augustine Okrah (84) na Maxi Mpia Nzengeli (85) yameifanya Yanga kuongoza kwa tofauti ya pointi 5 dhidi ya Azam FC inayoshika nafasi ya pili na pointi 10 dhidi ya Simba inayoshika nafasi ya Tatu.

Ihefu imebaki katika nafasi yake ya 8 katika msimamo ikiwa na pointi 23 katika michezo 20.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Kocha Mkuu wa Ihefu, Meck Mexime amesema; "Wala mambo yasiwe mengi, ni kweli tumeadhibiwa na timu bora leo sina hata neno lolote la kusema zaidi nawapongeza Yanga SC kwa kuzitumia nafasi walizozipata vyema.

"Kama utaona tumefungwa magoli mawili yote ya mpira ya kustukiza na sisi ndio tulikuwa golini kwako kuwashambulia ila wachezaji wangu wameshindwa kuzitumia nafasi, tumetengeza nafasi zaidi ya 4 tumeshindwa kuzitumia," amesema Mexine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: