Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mexime: Ihefu FC itatoboa Ligi Kuu

Mecky Mexime Ihefu Mexime: Ihefu FC itatoboa Ligi Kuu

Thu, 11 Jan 2024 Chanzo: Dar24

Kocha Mkuu wa Ihefu FC, Mecky Maxime amesema kikosi chake kina uwezo wa kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambao utaanza rasmi baada ya Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’.

Maxime amesema kama atapata ushirikiano mkubwa kutoka kwa uongozi wa timu hiyo na wachezaji kujituma zaidi ana uhakika wa kupata matokeo mazuri katika michezo iliyopo mbele yao na kuweza kujikwamua kutoka kwenye nafasi ya chini waliopo sasa kwenye msimamo wa ligi.

Maxime amesema ameiona timu yake na kwa sasa anafanya maboresho katika nafasi chache ili kutengeneza kikosi bora chenye kusaka ushindi katika michezo yake.

“Hatuwezi kujiondoa kwenye nafasi ya chini kama hatutakuwa na ushirikiano mzuri na wachezaji kupambana kutafuta alama tatu katika kila mechi zilizopo mbele yetu, kila mmoja wetu anatakiwa kujitoa katika mechi ili kupata matokeo mazuri mechi zetu zijazo,” amesema kocha Maxime.

Ameongeza kuwa baada ya kukabidhiwa timu ameanza programu ya mazoezi kwa kuweka falsafa zake hasa katika kipindi hiki ambacho Ligi Kuu imesimama kwa muda kupisha michuano ya ‘AFCON 2023’ inayotarajia kuanza Jumamosi (Januari 13), nchini Ivory Coast.

Amesisitiza hakutaka kuwapa muda wa kupumzika wachezaji wake kwa sababu anahitaji kupata muda wa kukaa na timu na kuanza kuingiza mifumo yake ili kikisuka kikosi chake kwa ajili ya duru la pili la Ligi hiyo.

Ihefu FC tayari imeshacheza mechi 14 za duru la kwanza imeshinda mechi tatu, imetoka sare mechi nne na wamepoteza michezo saba, wamekusanya pointi 13 wakishika nafasi ya 13 kwenye msimamo.

Chanzo: Dar24