Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mexico yatwaa ubingwa wa CONCACAF Gold Cup

CONCACAF Gold Cup.jpeg Mexico yatwaa ubingwa wa CONCACAF Gold Cup

Mon, 17 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya Mexico imeshinda kombe la kombe la dhahabu la CONCACAF (CONCACAF Gold Cup) 2023 kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Panama katika dimba la SoFi Los Angeles, Marekani kwenye FAINALI.

FT: Mexico 1-0 Panama

⚽ Santiago Gimenez 87'

Mexico imetwaa kombe Gold Cup kwa mara ya 9 ikiwa ndio Taifa lililotwaa taji hilo mara nyingi kuliko katika historia ya michuano ya CONCACAF. Marekani imetwaa mara 7 huku Canada ikitwaa mara moja.

SAFARI YA TIMU HIZI KWENYE CONCACAF GOLD CUP 2023

Mexico ilitinga fainali baada ya kuzifunga Honduras 4-0 na Haiti 3-1 lakini ikipoteza 1-0 dhidi ya Qatar kwenye kundi B, kabla ya kuitandika Costa Rica 2-0 kwenye robo fainali na kuiondosha Jamaica 3-0 kwenye nusu fainali.

Kwa upande wa Panama ilizifunga Costa Rica 2-1, Martinique 2-1 na kutoka sare ya 2-2 dhidi ya El Salvador kwenye kundi C, kabla ya kuikanda Qatar 4-0 kwenye robo fainali na kuiondosha Marekani kwa matuta 5-4 kwenye nusu fainali.

NB: Qatari imealikwa kwenye michuano ya Gold Cup 2021 na 2023 kama sehemu ya ushirikiano kati ya CONCACAF na Shirikisho la Soka la Qatar (QFA).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live