Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Metacha awatangazia vita washambuliaji Ligi Kuu

Metacha Polic Pic Data Golikipa wa Polisi Tanzania, Metacha Mnata

Thu, 21 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi Tanzania mpaka sasa imeshacheza michezo miwili na yote wamefanikiwa kuibuka na alama 3. Na hiyo ni kutokana na maandalizi mazuri ambayo wao kama timu walikuwa wakiyafanya kabla ya kuanza kwa msimu.

Sasa mlinda mlango wa Polisi Tanzania, Metacha Mnata amesema kazi ya soka haina kubahatisha na ndio maana anaamini katika ubora utakaompa neema ya kucheza timu yoyote.

“Mchezaji hukumu yake kama anajituma au la, ipo uwanjani kwa kile ambacho atakionyesha. Ndio maana nasisitiza kwamba uwezo ama ubora hauwezi kuchagua timu,” alisema Metacha.

Akizungumzia lengo lake msimu huu, amesema ni kuhakikisha anakuwa mwiba kuwanyima ujiko washambuliaji kuzifumania nyavu zake.

Kipa wa zamani wa Simba na Yanga, Said Mohamed ‘Nduda’ amesema kuwa: “(Metacha) ana kipaji. Kikubwa ajitume bila kuangalia ametoka Yanga, kwani kipaji kinawaka popote pale”.

Naye kocha wa makipa wa KMC, Fatuma Omary amesema kuwa alichokuwa anakifanya Metacha Yanga anapaswa kukiendeleza Polisi Tanzania ili afanikiwe zaidi.

Polisi Tanzania ilikua ishuke dimbani Oktoba 20 kupambana na Simba lakini kutokana na Simba kuwa na mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika, mechi hiyo imesogezwa mbele mpaka Oktoba 27.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live