Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Metacha atajwa kipigo cha Azam FC

METACHA.png Metacha atajwa kipigo cha Azam FC

Mon, 7 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KOCHA mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini ameweka wazi kuwa sababu kubwa ya ushindi wao wa juzi Jumamosi dhidi ya Azam ni ubora mkubwa aliokuwa nao kipa wao, Metacha Mnata katika kuokoa hatari zilizoelekezwa golini kwao. Juzi Jumamosi Polisi

Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, ushindi huo umeifanya Polisi Tanzania kufikisha pointi 22 zinazowaweka katika nafasi ya saba ya msimamo (kabla ya mchezo wa Geita Gold vs Yanga, jana Jumapili).

Kwenye mchezo huo, Metacha alionyesha kiwango bora na kufanikiwa kutoruhusu bao yaani ‘Clean sheet’, ambapo hii inakuwa Clean Sheet yake ya sita ndani ya Polisi Tanzania msimu huu.

Kocha Malale alisema: “Ulikuwa mchezo mzuri na mgumu kwetu hususan kwa kuwa tulikuwa na wachezaji wengi ambao walikuwa majeruhi, lakini jambo la muhimu ni kuwa tumefanikiwa kupata pointi tatu muhimu.

“Pia napenda kumpongeza kipa wangu Metacha Mnata ambaye ni wazi alikuwa kwenye kiwango bora Jumamosi, na naweza kusema bila yeye ingekuwa vigumu kupata ushindi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live