Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Metacha apigwa chini Yanga

Metacha Aliekuwa golikipa wa Yanga,Mtacha Mnata

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: Mwanaspoti

Kipa namba moja wa Yanga, Metacha Mnata amepewa mkono wa kwaheri kuitumikia timu hiyo baada ya leo Agosti 9 kukabidhiwa barua rasmi (Release letter).

Metacha mara ya mwisho kuonekana akiwa amevaa uzi wa Yanga ilikuwa ni Juni 17 mwaka huu kwenye mchezo wa Ligi dhidi ya Ruvu Shooting uliomalizika kwa timu yake kushinda bao 3-2.

Baada ya mchezo huo kumalizika kutokana na zomea zomea za mashabiki wakiamini kuwa hakudaka vizuri Metacha aliwatukana mashabiki wa Yanga kitendo ambacho sio cha kiungwana kwenye mchezo huo ambao ni burudani.

Kwa mujibu wa Meneja wa mchezaji huyo, Jemedari Said kupitia mtandao wake wa Instagram amethibitisha kuachwa kwa mchezaji huyo.

"Rasmi mabingwa wa historia nchini Yanga imeachana na golikipa wao namba moja Mnata," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Metacha alijiunga na Yanga SC mwaka 2019 akitokea Mbao FC ya Jijini Mwanza.

Chanzo: Mwanaspoti