Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Metacha amtimua meneja wake akihusishwa kurudi Yanga

Mnata Jemedar Metcha Mnata

Sat, 25 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Golikipa wa Polisi Tanzania Metacha Mnata amevunja mkataba na aliekuwa meneja wake Jemedari Said.

Tamko hili limekuja wakati huu ambapo metacha anazungumzwa kuhitajika na Yanga ambao wanampoteza Golikipa wao raia wa Mali Diarra anaekwenda kujiunga na Timu yake ya Taifa katika michuano ya AFCON.

Uhusiano wa Meneja huyo na Viongozi wa Yanga kwa siku za hivi karibuni umekuwa sio wa kuridhisha jambo linalowaacha wengi na maswali pengine ili aweze kurudi Yanga kwa urahisi basi golikipa huyo ameona ni vyema aachane na meneja wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live