Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Metacha ajitetea kipigo Kagame Cup

Metacha Gh Metacha ajitetea kipigo Kagame Cup

Thu, 11 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa wa Singida Black Stars, Metacha Mnata amedai kuwa licha ya kuiota fainali, michuano ya CECAFA Kagame Cup inampa mwanga kocha, Patrick Aussems kuandaa timu imara kwa msimu mpya wa mashindano ya Ligi Kuu Bara.

Metacha amesema michuano hiyo inawapa ushindani mkubwa na kuona makosa yao mapema na kocha wao kufanya kazi kwa kusahihisha madhaifu ambayo yanajitokeza katika michuano hiyo.

Singida Black Stars wameanza vibaya michuano hiyo kwa kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya APR ya Rwanda, mchezo uliochezwa jana usiku, katika dimba la Azam Complex lililopo Chamazi jijini Dar Es Salaam.

“Timu yetu ni mpya hata kocha naye, michuano hii anatumia kuangalia kikosi chake, kombinesheni ya wachezaji alikuwa nao, makosa yanayojitokeza ili kuja kutengeneza timu bora kwenye ligi itakapoanza,” amesema kipa huyo.

Ameongeza kuwa kupoteza mchezo huo kumetokana na makosa ya kimchezo yaliyofanyika na kudai kuwa wachezaji wengi hawana utimamu wa mwili na kutocheza muda mrefu hali iliyopelekea kutopata matokeo katika mchezo huo.

Metacha amesema benchi la ufundi wameona mapungufu na kufanyika kazi na kufanya vizuri katika michezo mwingine iliyopo mbele yao kwa kufikia malengo ya kuhakikisha kombe la CECAFA linasalia Tanzania.

Singida Black Stars inashuka dimbani kesho dhidi ya SC Villa ya Uganda, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jijini Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live