Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Metacha achafua tena hali ya hewa Yanga

Metacha Yanga Usajili Metacha achafua tena hali ya hewa Yanga

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa wa Yanga, Metacha Mnata ameshakitibua tena pale Yanga na sasa amewekwa kando na kikosi hicho kwa madai ya utovu wa nidhamu.

Inaelezwa kipa huyo ameingia kwenye utata wa nidhamu baada ya kushindwa kurejea kambini kwa wakati akitokea kambi ya timu ya taifa ‘Taifa Stars’ ilipocheza ugenini dhidi ya Algeria.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga ni kwamba Metacha hakufanya mawasiliano yoyote akiwa nje ya kikosi hicho na alianza kuwatafuta viongozi wa benchi la ufundi wakati Yanga ikiwa ugenini ilipopoteza dhidi ya Ihefu kwa mabao 2-1.

“Alipowatafuta viongozi ili arudi, tumeambiwa kocha (Miguel Gamondi), alizuia asirejee kwanza akichukizwa na kitu alichokifanya cha kukaa kimya huku wengine waliokuwa naye kwenye timu hiyo ya taifa wakiwa wamerudi,” alisema mmoja wa viongozi wa timu hiyo.

“Hatujajua amechukuliwa hatua gani, lakini kwenye timu ilikuwa bado hajarudishwa nadhani kuna mawasiliano anayafanya na viongozi kwanza.”

Mbali na Metacha inaelezwa pia kiungo Jonas Mkude, naye mapema alifanya kosa kama hilo ingawa alijiwahi na kujisalimisha na kupewa adhabu za ndani na baadaye kusamehewa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: