Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Metacha, Shikalo vita nzito Yanga

Vita Pic Data Metacha, Shikalo vita nzito Yanga

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Olipa AssaMore by this Author KIWANGO kinachoonyeshwa na makipa wa Yanga, Mkenya Farouk Shikhalo na Metacha Mnata ni kama wamemvuruga kocha wao wa makipa, Vladimir Niyonkuru kushindwa kujua nani atakuwa namba moja katika mechi za Ligi Kuu Bara.

Niyonkuru, raia wa Burundi alisema juzi baada ya Shikhalo kuonyesha kiwango bora katika michuano ya Kombe la Mapinduzi na Metacha kufanya vyema mechi za Ligi Kuu ni kama chemsha bongo kwao kushindwa kujua nani atakuwa anaanza na nani atasubiri.

Alisema japo ni nadra kuona nafasi ya makipa inabadilishwa mara kwa mara, lakini anaamini wote watatumika kwa manufaa ya klabu ili kuhakikisha ulinzi unakuwa mathubuti dhidi ya mashambulizi ya timu pinzani.

“Tunachokifanya tutawaangalia makipa hao kupitia mazoezi ili kujua mzunguko wa pili nani ataanza, hivyo atakayefanya vizuri zaidi atampa changamoto mwingine ya kujituma kuhakikisha ushindani unakuwa mkubwa,” alisema.

Niyonkuru alisema makipa wao wana mechi nyingi ambazo kila mmoja anaweza akatumika ipasavyo na pia ushindani wao ndio utafanya ukuta wao uwe na heshima katika msimu huu wanaotarajia kupata ubingwa kutokana na kuongoza ligi kwa pointi 44 mpaka sasa.

“Kila nafasi kwenye timu ikiwa na ushindani wa kutosha inasaidia kikosi kuwa bora zaidi, kwani anayetoka na kuingia viwango vyao vinakuwa vilevile, hiyo inakuwa inapunguza presha kwa kocha akiamini kikosi chake kipo na jeshi lenye kupambana na mazingira yote,” alisema Niyonkuru na kuongeza:

Chanzo: mwanaspoti.co.tz