Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Metacha, Mshery wanukia Azam FC

Metacha 3316 Metacha, Mshery wanukia Azam FC

Thu, 28 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Azam FC inatajwa iko katika mazungumo ya kumsajili golikipa wa Tanzania Prisons, Yona Amosi, kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi chao kwenye dirisha dogo la usajili.

Taarifa za ndani zinasema Yona amekuwa akihusishwa na Azam tangu tangu msimu uliopita kwa ajili ya kuchukua nafasi ya makipa waliopo, Abdulai Iddrisu na Ali Ahamada.

Hata hivyo pia Metacha Mnata na Abdultwalib Mshery, wote kutoka Yanga pia wanataja kuwa katika mazungumzo ya kujiunga na klabu hiyo tajiri hapa nchini.

Akizungumza na Nipashe, Ofisa Habari wa Azam, Thabiti Zakaria (Zaka), alisema wataongeza 'mtu hasa' katika nafasi ya kipa kwa sababu walinda mlango waliopo ni majeruhi na watakaa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Zaka alisema wako makini katika usajili watakaofanya na wanaamini watapata kipa mzuri na bora atakayeenda kusaidia kikosi chao ambaye huenda akatoka ndani au kutoka nje ya nchi.

“Tutaongeza wachezaji, kipaumbele chetu ni kipa kwa sababu tuliokuwa nao ni majeruhi wa muda mrefu, kipa wa kigeni si kipaumbele chetu bali tunahitaji nyanda mzuri kuja kusaidiana na makipa wetu kutoka timu ya vijana.

Kuhusu kipa wa Tabora United, John Noble, ni mkubwa sana na namhusudu sana. Lakini hayuko kwenye mipango yetu, na nyanda tutakaemsajili tutanuniwa na watu,” alisema Zaka.

Kuhusu maandalizi kuelekea mashindano ya Kombe la Mapinduzi, Zaka alisema kikosi chao kitaondoka jijini, Dar es Salaam leo kuelekea Zanzibar tayari kwenda kupambana kuwania taji hilo.

Azam watashuka dimbani kesho kuvaana na mabingwa watetezi, Mlandege mechi itakayochezwa kuanzia saa 10:15 jioni kwenye Uwanja wa Amaan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live