Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Metacha Ampa Jeuri Kocha Polisi Tanzania

Metacha?fit=1080%2C617&ssl=1 Metacha mnata, golikipa wa Polisi Tanzania

Thu, 7 Oct 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania, Malale Hamsini, ameweka wazi kuwa usajili bora wa vijana walioufanya akiwemo mlinda mlango, Metacha Mnata, ndiyo sababu ya kuwa na timu bora ambayo anaamini itawashangaza wengi msimu huu.

Metacha aliyesajiliwa na Polisi Tanzania baada ya kuachwa na Yanga, tayari amedaka katika mechi mbili za Polisi Tanzania na zote wameshinda.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Malale amesema: “Tunashukuru kwa kuanza msimu vizuri na kufanikiwa kushinda michezo miwili ya kwanza, kwangu haya ni matokeo ya kufanya usajili mzuri hasa wa vijana wadogo na wenye uwezo mkubwa kama kipa wetu Metacha Mnata.

“Kutokana na uwepo wa vijana wengi kwenye kikosi chetu, unaweza kuona timu imekuwa na kasi kubwa, ukiangalia mabao yote manne tuliyofunga katika michezo miwili iliyopita ilitokana na uwezo mkubwa wa kufanya mashambulizi ya kushitukiza, naamini kama tutaendelea hivi basi tunaweza kumaliza nafasi nzuri zaidi msimu huu.”

Chanzo: globalpublishers.co.tz