Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Metacha: Al Ahly watakutana na saparaizi nzito kesho

Metacha Bacca Job Mudathir 0003 Metacha: Al Ahly watakutana na saparaizi nzito kesho

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa wa Yanga SC, Metacha Mnata amezungumzia utofauti wa Yanga iliyocheza na Pyramids mwaka 2019 na hii ya sasa.

Metacha ndiye mchezaji pekee aliyesalia kwenye kikosi cha wananchi ambacho kilicheza mchezo wa mwisho nchini Misri 2019.

Katika hatua nyingine amemtaja mchezaji anayemkumbuka zaidi kwenye kikosi cha Yanga iliyocheza na Pyramids FC mwaka 2019 Jijini Cairo Misri.

"Wakati ule kikosi kilikuwa sio kama cha sasa, wakati huo walikuwa wanahangaika kutafuta wachezaji na kuijenga timu ili kupata timu bora na iliyoimarika. Hata uongozi wa zamani ni tofauti na wa sasa.

"Kwa sasa uongozi uko imara, timu imesimama na imeimarika ina uwezo wa kucheza kokote kule iwe ndani au nje ya Tanzania. Timu imeimarika kila idara, niwaambie tu Al Ahly watakutana na sapraizi kubwa sana Ijumaa.

"Kipindi kile tulikuwa na Haruna Niyonzima, nimemmiss mpaka leo. Kikubwa wananchi watuombee tupate ushindi," amesema Metacha.

Yanga SC ipo tena nchini humo kwaajili ya kucheza dhidi ya Al Ahly Ijumaa hii saa 1:00 usiku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live