Kocha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Scaloni amesema kua nahodha wa timu hiyo Lionel Messi ndio ataamua hatma yake ndani ya timu hiyo kama anaendelea kuichezea timu hiyo au anastaafu.
Kocha Scaloni anaamini Messi ataendelea kuitumikia timu hiyo kwa miaka kadhaa mbele kwani amesema hatma ya mchezaji huyo ipo mikononi mwake, Lakini haoni staa huyo akiachana na timu ya taifa ya Argentina siku za usoni licha ya kushinda kila taji na timu hiyo.
Scaloni alieleza kua baada ya michuano ya Kombe la Dunia staa huyo alitabiriwa ataendelea kuitumikia timu ya taifa ya Argentina, Mpaka sasa kocha huyo anaamini staa huyo ataendelea kuwepo timu hiyo mpaka yeye mwenyewe aamue kuachana na timu hiyo.
Kocha huyo ameeleza anafurahia uwepo wa Messi kwenye timu ya taifa ya Argentina kwa sababu bado anaonekana yuko vizuri, Vilevile kocha huyo amesema mchezaji anastahili kuendelea kuichezea timu hiyo kutokana na ubora ambao amekua nao kwasasa.
Kocha Scaloni amewahakikishia wanahabari kua Messi ataendelea kuonekana kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Argentina mpaka pale mwenyewe atakapoamua kuachana na timu hiyo, Timu ya taifa ya Argentina itacheza mchezo wa kirafiki wiki hii kwa mara ya kwanza dhidi ya Panama baada ya kutwaa kombe la dunia.