Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messi ndio basi tena Barca

Lionel Messi Messi ndio basi tena Barca

Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Barcelona usiku wa leo wamethibitisha staa wao Lionel Messi hataongeza mkataba wa kusalia kikosi hapo baada ya kushindwana kwenye mambo mawili.

Barcelona wamethibitisha kupitia mtandao wao kuwa mazungumzo yalianza vizuri na walikaribia kusaini mkataba ila sasa wameshindwana kwenye fedha na mfumo.

"Ilibidi tusaini mkataba mpya leo, ila haitawezekana kwasabu za masuala ya kifedha na kimfumo ambao ni sheria za La Liga," imeeleza taarifa hiyo.

Mkataba wa Messi uliisha June 30 mwaka huu na sasa anakuwa mchezaji huru ambaye alikuwa anawindwa na Manchester City.

Barca wamemtakia kila la kheri nyota huyo ambaye alikuwa kivutio cha ligi ya Hispania na mshindi mara sita wa Ballon d'Or huku wakisikitika kutotimiza yale Messi aliyataka.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz