Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messi kurudi Barcelona

Lionel Messi Miami Lionel Messi

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha na Mshambuliaji wa kikosi cha Argentina Lionel Messi ameahidiwa kufanyiwa jambo la kipekee ili kuaga rasmi ndani ya Barcelona pindi atakapofikia mwisho wa maisha yake ya soka.

Jorge Mas, ambaye anamiliki Klabu ya Inter Miami sambamba na David Beckham na Jose Mas, alisema amempa gwiji huyo ahadi yake kwamba atafanya kila linalowezekana kukamilisha jambo hilo kwa staa huyo anayeitumikia klabu hiyo hivi sasa.

“Messi alipoondoka Barcelona hakuweza kuiaga klabu yake ambayo ilimkaribisha akiwa mtoto, nadhani mazingira hayakuwa yale ambayo Lionel alitaka,” alisema kiongozi huyo na kuongeza.

“Nilimpa [Messi] ahadi yangu kwamba nitafanya kila niwezalo katika miaka ijayo ili apate fursa ya kuwaaga mashabiki wake huko Barcelona.

“Inter Miami itakwenda (kwa Barcelona) au tutakuwa na aina fulani ya mechi.”

Messi alidumu ndani ya Barcelona kwa kipindi cha takribani miaka 20 baada ya kujiunga na klabu hiyo akiwa na miaka 13, akaondoka mwaka 2021 na kutua PSG, kabla ya 2023 kujiunga na Inter Miami.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live