Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messi kuondoka Miami? bado yupo sana tu

Lionel Messi 1692504890 114379 Messi kuondoka Miami? bado yupo sana tu

Fri, 13 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Nyota wa Inter Miami Lionel Messi amefanya uamuzi wake juu ya uhamisho wake katika usajili wa dirisha dogo la Januari kwa mujibu wa ripoti.

Nyota huyo amekuwa akihusishwa na uhamisho wa mkopo kwenda Barcelona au katika klabu moja ya Saudi Arabia.

Msimu wa Ligi Kuu Marekani unakaribia kuisha na timu inayomilikiwa na David Beckham inatazamiwa kukosa mechi za kufuzu za 'play-off'.

Kulikuwa na uvumi kwamba Messi anaweza kuchukuwa likizo ya muda mrefu hadi mwakani ndio maana kuna uwezekano akaondoka kwa mkopo.

Lakini gwiji wa masuala ya usajili Fabrizio Romano amedai kwa sasa hafikirii kujiunga na timu nyingine na inasemekana anaiangazia zaidi klabu yake ya Inter Miami na timu ya taifa ya Argentina.

Timu yake ya taifa itamenyana na Paraguay, Peru, Uruguay na wapinzani wao Brazil katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 katika muda wa miezi miwili ijayo.

Mechi za kujiandaa na msimu wa Inter Miami zitaanza Januari, lakini Messi anaweza kucheza mechi za kirafiki na inatazamiwa kufanyika katika bara la Asia mwezi ujao kabla ya mapumziko ya mwezi mzima.

Barcelona inadaiwa kuwa tayari kumrudisha gwiji huyo mwenye umri wa miaka 36 licha ya matatizo ya kifedha inayokabiliwa nayo.

Wakati huohuo, Messi alikataa kusaini mkatabaa wenye thamani ya Pauni 350 kutoka Al-Hilal katika dirisha la usajili la kiangazi lililopita. Badala yake walimsajili mchezaji mwenzake wa zamani wa Barcelona Neymar.

Chanzo: Mwanaspoti