Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messi kumfuata Ronaldo Saudia

Messi Si Rafiki Yangu Lakini Namheshimu   Christiano Ronaldo.png Messi kumfuata Ronaldo Saudia

Sat, 2 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Inter Miami imeripotiwa kuipotezea mechi ya kirafiki dhidi ya Flamengo kutoka Brazili kwa ajili maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Marekani na imepanga kwenda Saudi Arabia.

Taarifa zimeripoti, Inter Miami imetangaza mechi za kirafiki dhidi ya timu kutoka Saudi Arabia ikiwemo Al-Nassr ya Cristiano Ronaldo.

Timu hiyo inayomilikiwa na David Beckham itafanya ziara duniani kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya ya kampeni ya MLS.

Awali Inter Miami imekanusha makubaliano ya mechi yoyote ya kirafiki dhidi ya Al-Nassr baada ya kudaiwa inaweza kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu hiyo.

Sasa uwezekano wa Ronaldo na Messi kupambanishwa ni jambo linalotarajiwakwa sasa kwa mujibu wa taarifa hiyo.

Messi na Ronaldo wamekutana mara 36 katika maisha ya soka, huku mechi ya kwanza baina yao ilikuwa mwaka 2008.

Katika mechi hizo walizokutana Messi ameshinda mara 16  dhidi ya 11 za Ronaldo kwa kipindi hicho chote, mbali na mchuano wao wa kuwania na kubeba tuzo mbalimbali za soka.

Mastaa wa Inter Miami wanafurahia mapumziko baada msimu kumalizika na wanatarajiwa kujiandaa na msimu mpya wa mwaka 2024.

Ingawa ratiba haijathibitishwa, inaonekana Inter Miami ina malengo makubwa kuelekea msimu mpya wa Ligi ya Marekani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live