Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messi hajamsaliti mkewe

Messi X Wife Lionel Messi na mkewe Antonela Roccuzzo

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mke wa nyota wa zamani wa Arsenal, Cesc Fabregas, Daniella Semaan amekanusha vikali ripoti nchini Brazil inayodaiwa kuwa Lionel Messi amemsaliti mke wake Antonela Roccuzzo.

Gazeti la Brazil Direto Do Miolo lilichapisha kupitia akaunti ya X Ijumaa kwamba uhusiano wa Messi na Roccuzzo uliodumu kwa miaka 15 unakabiliwa na mgogoro kati yao.

Imedaiwa kuwa nyota huyo wa Inter Miami alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwandishi wa habari kutoka Argentina, Sofia Martinez huku ndoa yao ikiwa hatarini kuvunjika.

Lakini taarifa hizo zimepingwa vikali kutoka kwa vyombo vya habari Hispania na Mbaya zaidi rafiki wa karibu na familia hiyo Daniela, ambaye mara kwa mara wanakuwa pamoja na Messi na Antonella amekanusha vikali uvumi huo ambao sio wa kweli.

Messi na Roccuzzo wamefahamiana tangu wakiwa na umri wa miaka mitano na walifunga ndoa mwaka 2017 na kubahatika kupata watoto watatu Thiago, Mateo na Ciro.

Ripoti nchini Argentina ziliibuka mwezi uliopita zikithibitisha Messi amemsaliti kipenzi chake wa muda mrefu, na baadhi ya mashabiki wakahisi kweli mwanahabari huyo alihusika na staa huyo, kutokana na dalili alizomwonyesha wakati anamhoji kwenye sherehe ya Ballon d’Or.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live