Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messi bado majanga tu

Messi Final Messi bado majanga tu

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Nyota wa Inter Miami Lionel Messi ataendelea kuwa nje ya dimba kutokana na maumivu ya misuli kwa mujibu wa ripoti na pigo kwa klabu hiyo.

Messi alikosa mechi ya ligi dhidi ya NYFC iliyochezwa wikiendi iliyopita kutokana na majeraha hayo ambayo yamemfanya kukosa mechi nne katika mechi tano za mwisho za Inter Miami.

Mechi pekee ambayo hakukosa ilikuwa dhidi ya Toronto ambayo alicheza dakika 37 mwezi uliopita. Staa huyo alifanyiwa mabadiliko kabla ya mapumziko kwa sababu ya kile kinachoaminika kuwa alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya misuli.

Messi alirejea dimbani baada ya mechi za kimataifa za kufuzu Kombe la Dunia akiwa na kikosi cha Argentina lakini sasa atakuwa nje kwa muda mrefu.

Inter Miami ilikuwa nyuma kwa pointi tano dhid ya NYCFC huku ikiwa na mechi mbili mkononi. Timu hiyo ilisaka ushindi kujiweka katika nafasi nzuri katika mchujo zinazojumuisha timu tisa.

Wakati huo huo Inter Miami ilituma taarifa la ongezeko kubwa la bei za tiketi kwa ajili ya msimu ujao. Bei hizo zimepangwa kupanda kwa asilimia 82 (kutoka Dola 485 hadi Dola 884) kwa mwaka wa 2024.

Bei ya baadhi ya viti itapanda kwa asilimia 98 (kutoka Dola 1,333 hadi Dola 2,635) tofauti ilivyokuwa msimu huu.

Chanzo: Mwanaspoti