Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messi awaliza Lepzig, PSG ikishinda nyumbani

Mess Lionel La Pulga Lionel Messi akijaribu kuwatoka wachezaji wa Lepzig

Wed, 20 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matajiri wa Jiji la Paris, klabu ya Paris Saint-Germain wameibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya RB Leipzig katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Parc des Princes Jijini Paris, Ufaransa.

Nyota wa mchezo alikuwa ni mshambuliaji Muargentina, Lionel Messi aliyefunga mabao mawili dakika ya 67 na lingine 74 kwa penalti ya panenka baada ya Kylian Mbappe kufunga la kwanza dakika ya tisa ya mchezo.

Mabao ya RB Leipzig yalifungwa na Andre Silva dakika ya 28 na Nordi Mukiele dakika ya 57 na kwa ushindi huo PSG inarejea kileleni ikifikisha pointi saba, moja zaidi ya Manchester City baada ya wote kucheza mechi tatu.

RB Leipzig imefungwa mechi zote tatu na inashika mkia mbele ya Club Brugge yenye pointi nne.

Messi ambae kiwango chake tangu ahamie PSG kimekuwa hakiwaridhishi walio wengi usku wa jana alionekana kung'ara katika mchezo huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live