Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messi atumiwa ujumbe wa vitisho, risasi zapigwa dukani

Messi Shambuliwaaa Messi atumiwa ujumbe wa vitisho, risasi zapigwa dukani

Fri, 3 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa Soka kutokea nchini Argentina, Lionel Messi (35) ametumiwa barua ya vitisho baada ya watu wenye silaha kushambulia duka kubwa linalomilikiwa na familia ya mke wake Antonela Roccuzzo (35) jijini Rosario, nchini Argentina, AFP wanaripoti.



Kwa mujibu wa maelezo ya Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea mapema jana saa tisa alfajiri, Watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki walifyatua takriban risasi kumi na nne kwenye madirisha ya duka la Unico liliko jijini Rosario.

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi hakuna aliyejeruhiwa katika eneo la tukio ingawa kulikuwa na uharibifu uliofanyika kwenye duka hilo huku barua ya vitisho iliachwa na ikiwa imeandikwa "Messi, tunakusubiri! Javkin ni muuza madawa ya kulevya, hatokusaidia.", Javkin ndiye Meya wa jiji la Rosario, nchini Argentina.



Meya wa Rosario Pablo Javkin ameripotiwa kufadhaika na tukio hilo huku akisema jambo hilo limeleta ongezeko la ghasia na wasiwasi jijini humo, mpaka sasa, Messi pamoja na mke wake Antonela Roccuzzo hawajazungumzia tukio hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live