Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messi atambulishwa rasmi kwa mashabiki wa Miami

Messi Atambulishwa Rasmi Kwa Mashabiki Wa Miami Messi atambulishwa rasmi kwa mashabiki wa Miami

Mon, 17 Jul 2023 Chanzo: Voa

Lionel Messi amewasilishwa rasmi kwa mashabiki wa Inter Miami katika uwanja wa DRV PNK.

Umati uliokuwa umenunua tiketi watu takriban 20,000 ulisubiri licha ya kuwa na mvua ya radi kumwona mshindi huyo mara saba wa Ballon d'Or akipewa jezi namba 10.

Katika hotuba fupi ya Kihispania, Messi, 36, aliwashukuru wafuasi na kusema alikuwa na "hamu sawa" anayokuwa nayo kila wakati.

Mshambuliaji huyo wa Argentina aliyeshinda Kombe la Dunia anajiunga na klabu ya Ligi Kuu ya Soka kwa mkataba hadi mwisho wa 2025.

Ataunganishwa tena na kiungo wa kati Sergio Busquets - ambaye alicheza naye Barcelona - ambaye pia amesajiliwa Miami hadi 2025.

Busquets, pia, alizinduliwa rasmi wakati wa tukio la Jumapili usiku.

Messi aliingia uwanjani kwa kutembea kwa miguu na kutambulishwa kama "Nambari 10 wa Marekani, bora zaidi duniani".

Mshindi mara saba wa Super Bowl Tom Brady na bingwa mara nne wa NBA Stephen Curry pia walimkaribisha Marekani kwa jumbe za video.

"Ninataka sana kuanza mazoezi, kushindana," Messi alisema.

"Nina hamu kama ile ambayo siku zote nilikuwa nayo kushindana, kutaka kushinda, kusaidia klabu kuendelea kukua.

"Nina furaha sana kuchagua kuja kucheza katika jiji hili na familia yangu, kuchagua mradi huu na Sina shaka kuwa tutaifurahia sana.

"Tutakuwa na wakati mzuri na mambo mazuri sana yatatokea."

Uwanja wa DRV PNK ulioko Fort Lauderdale ni uwanja wa muda wa Inter Miami na una uwezo wa kubeba watu 18,000, na kuufanya kuwa uwanja mdogo zaidi wa MLS pamoja na PayPal Park ya San Jose Earthquakes huko California.

Jumba kuu la muda limejengwa ili kuruhusu mashabiki zaidi uwanjani.

Messi aliwaacha mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain mwishoni mwa msimu wa 2022-23 baada ya kufunga mabao 32 katika michezo 75 katika kipindi cha miaka miwili.

Alikataa ofa nono kutoka nchi nyingine kwenda kucheza Marekani - na hii ni mara yake ya kwanza kuchezea klabu isiyo ya Ulaya.

Mmiliki mwenza wa Inter Miami David Beckham alisifu usajili wa Messi kama "ndoto iliyotimia".

“Leo, tunajivunia kwamba umechagua klabu yetu kwa hatua inayofuata katika taaluma yako ya soka,” alisema.

Mmiliki mkuu wa Inter Miami, bilionea wa Marekani Jorge Mas, alimtaja Messi "mchezaji bora zaidi kuwahi kuvaa buti".

Messi anatarajiwa kuwepo kuichezea Miami dhidi ya timu ya LIGA MX Cruz Azul tarehe 21 Julai katika mechi yao ya ufunguzi ya Kombe la Ligi.

Chanzo: Voa