Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Messi apiga za fasta fasta Marekani

Messi 500 Goals Lionel Messi

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Supastaa, Lionel Messi ameweka rekodi kwenye Ligi Kuu Marekani baada ya kuwa mchezaji aliyetumia muda mfupi zaidi kuhusika kwenye mabao 25 katika msimu wake mmoja kwenye mikikimikiki hiyo.

Mshindi huyo mara saba wa Ballon d’Or alijiunga na Inter Miami muda mfupi baada ya kutoka kunyakua Kombe la Dunia 2022 akiwa na kikosi cha Argentina kwenye fainali hizo zilizofanyika Qatar.

Miami ilishindwa kufanya vizuri kwenye mechi za mchujo katika msimu wake wa kwanza wa Messi kwenye timu hiyo, lakini safari hii timu hiyo ni vinara kwa upande wa Eastern Conference. Na kinachovutia, Messi, 36, amefunga mabao 12 na kuasisti 13 katika msimu huu na kufikisha idadi hiyo kwa haraka zaidi, akiwa amecheza mechi 12 tu.

Awali rekodi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na staa wa zamani wa Arsenal, Carlos Vela, aliyoweka mwaka 2019, ambapo alihitaji mechi 16 kuhusika kwenye mabao 25. Rekodi hiyo ya Messi imekuja baada ya kuifungia Inter Miami bao la kwanza kwenye sare ya 3-3 dhidi ya St Louis City, Jumamosi. Mastaa kadhaa wanajiandaa kwenda kuungana na Messi kwenye kikosi hicho cha Inter Miami, huku tayari mastaa wenzake wa zamani wa Barcelona, Luis Suarez, Sergio Busquets na Jordi Alba wanapiga mzigo pamoja.

Suarez na Alba ni wachezaji wengine waliofunga mabao katika mechi hiyo ya Jumamosi. Na sasa, Messi imehamishia akili yake kwenye michuano ya Copa America, ambayo itakayoanza Juni 21.

Chanzo: Mwanaspoti